Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,509
- 3,992
Wakuu
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, ugomvi wa ngumi umezuka nje ya Ukumbi wa Ubungo Plaza unapofanyika mkutano wa uchaguzi wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha).
Ugomvi huo ulikuwa kati ya wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu dhidi ya wafuasi wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Soma, Pia: Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025
Ingawa mkutano huo wa uchaguzi ulioanza mchana wa jana Alhamisi, Januari 16, 2025 unaofanyika ni wa wanawake, lakini waliorushiana ngumi walikuwa wanaume.
Chimbuko la ugomvi huo ni mabishano ya kuimarishwa kwa ulinzi, yaliyosababisha kutiliwa shaka mmoja wa watu waliokuwepo katika lango kuu la Ukumbi wa Ubungo Plaza.
Mabishano hayo, yalisababisha walinzi kuanza kumuondoa mtu huyo na wengine waliokuwepo eneo hilo na kuanzia hapo watu walianza kushambuliana.
PICHA: Mwananchi
Pia, Soma:
- VIDEO: Mbowe, Lissu wasalimiana kibabe BAWACHA, huku wakicheza kwa bashasha wimbo wa "Tuvushe Mbowe Tuvusheee"
- Video: BAWACHA wamuunga mkono Tundu Lissu hadharani, wasema "Mabadiliko lazima"