Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,635
- 29,509
Wadau,
Mimi ni mteja wa Vodacom na kutokana na Biashara zangu z Hapa na pale hua nafanya pia Biashara na Kenya na mara nyingi natumiaga M-pesa kutuma hela Kenya kisha natumiwa Bidhaa. Nimefanya miamala mingi tu na Kenya ila leo nimewaza hii biashara nayoifanya nikagundua kama sio wizi wa Vodacom ningekua Mbali zaidi.
Vodacom wanachaji kiasi cha TZS 23.76 kwa kila 1KES unapokua unatuma pesa Kenya. Kiwango hiki ni kikubwa mno kulinganisha na bei ya kwenye Maduka ya fedha (Bureau de Changes). Mfano nikitaka kutuma KES 100,000 basi kwa kutumia Mpesa nitahitajika kutumia Tshs 2,376,000/= wakati kwenye maduka ya fedha ambako nanunua KES 1 kwa Tshs 21.5 ningelipa Tshs 2,150,000/= (hasara 226,000/=). Hii ni zaidi ya Faida nayoipata kwa mzigo naoulipia hizi hela.
Na serikali hapa pia inapoteza hela nyingi sana, maana ki ukweli hii ni biashara ya Bureau De Change "bubu" wanafanya hawa Vodacom. Ukiacha fact kwamba wanatuibia kwa kutukata rate kubwa, pia wanaiibia serikali kwa kufanya biashara ya Bureau de Change Bila Kibali.
Naomba mamlaka zinazohusika na mambo haya ziangalie hili swala, tulipishwe kwa rate ya Soko, pia Hawa Voda ikiwezekana wasajiliwe kama Bureau de Change nao walipe kodi pia kwenye sekta hiyo