Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Naaam kumekucha..Ule mfululizo wa patashika ya kumtafuta bingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2019/2020, Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kutimua vumbi leo Jumapili ya Novemba 3, 2019 katika viwanja tofauti nchini, ambapo JKT Tanzania watamenyana na Tanzania Prisons huku Coastal Union wakiwa Uwanja wa Mkwakwani Stadium wakiwakabili Mbao FC.
Kazi ipo Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, ambapo bingwa mtetezi Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni, baada ya kutoka kujeruhiwa katikati ya wiki na Mwadui FC kwa kupoteza mchezo kwa kufungwa 1-0 atasimama upya mawindoni kuzisaka alama tatu muhimu zitakazo mwezesha kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa VPL kwa kukipiga dhidi ya Mbeya City.
••Kulitaka Mwana...Kulipewa Mwana.
Wanasimba na mdau wa kandanda karibu uwanja wa Uhuru kushuhudia huu mtanange wa kukata na soka wa VPL, hasa soka la kiwango cha CAF kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi.
Usikose ukaambiwa..Kumbuka michezo yote ni kuanzia saa 10:00 jioni.
SimbaNguvuMoja..Next Level
•••••=============•••••
Klabu ya Simba SC wameweza kutakata uwanja wa Uhuru baada ya kuibuka na ushindi mnono kwa kuichapa Mbeya City mabao manne bila majibu yakiwekwa kimiani na Kagere 8' Chama 43' Shiboub 78' Deo Kanda 87' VPL.
FT: Simba SC 4-0 Mbeya City