Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 240
- 1,141
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imesema imepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wateja kuhusu vikomo vya malipo na miamala kwa akaunti za M-Pesa.
Kupitia taarifa yake kwa Umma, kampuni hii imetoa taarifa kuwa M-Pesa Limited inafanya kazi chini ya leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuzingatia Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Kitaifa ya 2015 Udhibiti wa Pesa za Kielektroniki. Kulingana na sheria, kuna vikomo vya miamala ya kila siku kwa kiasi ambacho mtu binafsi anaweza kutuma na kupokea kulingana na utimilifu wa mahitaji ya KYC.
Pia soma: Inakuaje akaunti ya M-Pesa ya CHADEMA inasema pesa zimejaa wakati kwenye makubaliano Vodacom ilisema akaunti haina ukomo?
Vikomo vya miamala vinavyotumika vimewekwa chini ya Sheria ya Mfumo wa Malipo wa Kitaifa ya 2015 Kanuni za Pesa za Kielektroniki zinazotolewa na BoT. Kanuni hizi zinatumika kwa miamala yote ya M-Pesa na pia kwa waendeshaji wengine wa pesa za simu nchini Tanzania.
Mapema Machi 1, 2025, zilisambaa taarifa kwenye Mtandao wa X zikidai kampuni hiyo imepokea maelezo kutoka Serikalini kuzuia miamala ya fedha inayotumwa kwenye namba ya Vodacom ya CHADEMA ili kukwamisha kampeni ya kuchangisha pesa inayoendeshwa na chama hicho.
Miongoni mwa watu waliotoa madai hayo ni Mbunge wa zamani wa Arusha, Godbless Lema, Mwanaharakati Maria Sarungi pamoja na wadau na wapenzi wengine wa CHADEMA.