VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,060
5,446
Tanzania na Ethiopia zimesaini mikataba kadhaa na Korea Kusini kwa ajili ya kupata mikopo ya mabilioni ya dola kwa ajili ya maendeleo.

Mikopo hiyo itaiwezesha Korea Kusini kupata fursa ya kuchimba madini muhimu katika nchi za Afrika.

Korea Kusini imeandaa kongamano na viongozi 30 wa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania na Ethiopia.

Kongamano linafanyika wiki hii

Tanzaia imesema kwamba itakopa dola bilioni 2.5 kutoka kwa Korea Kusini katika muda wa miaka mitano ijayo. Mkopo huo utalipwa katika muda wa miaka 5.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan vile vile amesaini mkataba utakaoiruhusu Korea Kusini kutumia bahari yake na madini yanayotumika katika teknolojia ya nishati safi kama Nickel, Lithium na Graphite.

Ethiopia nayo imesaini mkopo wa dola bilioni 1 utakaolipwa katika kipindi cha miaka minne kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu, sayansi na teknolojia, afya na maendeleo ya mijini.

PIA SOMA
- Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51

- Prof. Kitila Mkumbo akanusha masharti ya Mkopo wa Korea Kusini

- Balozi wa Tanzania nchini Korea akanusha upotoshaji Tanzania kutoa sehemu ya Bahari na Madini

Voice of America
 
The way forward is to warn those would be investors kuwa haya yanafanyika bila ridhaa ya watanzania, kesho tutawafukuza maana wameletwa na swaiba wao na si watanzania

Najua mikataba ya kimataifa si rahisi kuivuja, but let the International community know this. Give them a warning , Wanaharakati/wanasheria wanaweza kuitaarifu dunia kuwa anachokifanya Samia hakina ridhaa ya watanganyika.
 
The way forward is to warn those would be investors kuwa haya yanafanyika bila ridhaa ya watanzania, kesho tutawafukuza maana wameletwa na swaiba wao na si watanzania
Hakuna kitu kama hicho, serikali iki sign mkataba serikali zjazo zinakuwa hooked na lazima mlipe hata kama mkataba ilikuwa ya hovyo, Hilo ni tatizo lenu sio lao, only thing ni kuwashtaki viongozi walio sign hiyo mikataba hata deni litalipwa tuu
 
Najua sana hilo, but you can give a warning! wajue kuwa hawana ridhaa ya wananchi. Let the international community get informed of that rubbish
 
Back
Top Bottom