Vitu 3 muhimu vya kuwa navyo unapoomba Kitambulisho cha Taifa (NIDA)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,362
13,001
1719233455739.jpeg

JamiiForums, imezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Geofrey Tengeneza kufahamu iwapo wameongeza nyaraka za kukabidhi ili kupata Kitambulisho cha Taifa (NIDA) ambaye ameeleza kuwa taarifa hiyo haina ukweli na siyo sahihi.

"Hiyo siyo kweli na siyo sahihi kabisa, vitu va msingi kabisa kwa jaili ya kusajili kupata kitambulisho cha NIDA ni:-

Cheti cha kuzaliwa cha mtu anayeomba analeta nakala
Cheti cha kuzaliwa(nakala) cha mzazi mmojawapo, baba au mama, na kama hawana hicho cheti cha kuzaliwa kama wana kitambulisho cha NIDA cha mzazi mmjowapo baba au mama basi unaambatanisha nakala ya cheti cha NIDA cha mzazi mmojawapo baba au mama. Na kama hawana vyote hivyo cheti cha kuzaliwa au nakala ya NIDA basi unakwenda kwa mwanasheria au mahakamani, anakupa kiapo unaapa kwa jina kinaitwa affidavit kwa ajili ya mzazi mmoja wapo, unaapa kisha unaambatanisha hiyo affidavit.

Kitu cha tatu cha msingi ni barua ya Serikali za mtaaa unakoishi, kwa hiyo lazima uwe na barua ya Serikali za mtaa unakoishi wanaeleza kwamba wanakutambua kama mkazi katika huo mtaa katika lile eneo.

Kwa hiyo hivi ndio vitu vitatu vya msingi sasa hivi vitu vingine vitu unaweza ukaambiwa kama cheti cha mpiga kura nakala, ama leseni ya udereva, cheti cha elimu ya msingi au sekondari hivi ni vitu vya nyongeza tu ili kutia uzito maombi yako, lakini siyo vitu vya msingi, lakini haina maana kama ukiwa huna hivyo hautasajiliwa, hata kama huna hivyo na unavyo vile vitu vitatu vya msingi, kama cheti cha kuzaliwa, checti cha kuzaliwa cha mzazi au kadi yake ya NIDA au affidavit na barua ya serikali za mtaa basi utasajiliwa tu.

Hivo vitu vingine ni vitu tu vya kuongeza kama utakuwa navyo mwenyewe kutia nguvu maombi yako na si kwamba kama utakuwa hauna hiyo vya kuongezea hautasajiliwa hiyo si kweli, hata kama huna hivyo vya kuongezea utasajiliwa tu". Geofrey Tengeneza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

Pia soma: NIDA mmeongeza nyaraka za kukabidhi ili kupata Kitambulisho cha Taifa. Hii ni halali kweli? | NIDA wafafanua, wataja vitu vitatu muhimu kuwa navyo
 
Back
Top Bottom