nameless girl
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 4,195
- 2,674
Habari zenu wakuu?
Kwa wale wapenzi wa riwaya mbalimbali hususani vye marehemu Bne Mtobwa sasa vinapatikana. Vitabu hivyo ni pamoja na mfululizo wa vitabu vya Joram Kiango na vitabu vingine vya kijamii. Vitabu hivyo ni kama vifuatavyo...
1. KIGUU NA NJIA
Hiki ni kitabu ambacho kinabeba historia ya nchi yetu kwa njia ya simulizi.
Inamuhusu kijana Kionambali, Muha toka Kigoma ambaye alitakiwa kuuawa ili kuleta mvua kutokana na mila potofu ya kwao. Jambo hilo lilimfanya babu yake kumshauri kuondoka katika eneo hilo kwa nia ya kuepuka kifo lakini pia aweze kutafuta elimu ambayo kwa kipindi hiko ilikuwa ikitolewa na mtu mweupe.
Jambo hilo linamfanya Kionambali afike sehemu mbalimbali ambazo ni mafunzo kwa msomaji wa kitabu hiki.
Kinapatikana kwa bei ya shilingi 15,000 za Kitanzania.
2. MIKATABA YA KISHETANI
Hiki ni kitabu kinachomuhusu mpelelezi Joram Kiango ambapo msichana anayefanya kazi serikalini anauawa na muuaji anapewa maelekezo ya jinsi ya kumuua msichana huyo na kupewa hata nguo atakazovaa siku hiyo jambo ambalo linamfanya hata muuaji mwenyewe atamani kumjua bosi wake aliyemtuma kumuua msichana huyo.
3. SALAMU TOKA KUZIMU
Kitabu hiki pia kinamuhusu mpelelzi Joram Kiango ambaye anauawa na bomu na kisha kuleta salamu toka kuzimu kwa muuaji wake.
4. Dar es salaam usiku
Ni riwaya inayoelezea maisha ya vijana wasio na elimu wala kazi wanapopambana na maisha kwa njia ambazo si nzuri ila kwao ndio chanzo cha wao kuendelea kuishi kwa kujipatia chochote kwa njia hizo.
5. MTAMBO WA MAUTI
Ni kitabu kinachomuhusu msichana ambaye ni mwandishi anayempelekea kazi zake Joram Kiango kwa ajili ya kupata ushauri lakini anauawa akiwa chumbani mwa Joram Kiango kisha Joram anapokuwa anatafutwa na askari kwa ajili ya mauaji hayo, msichana huyohuyo anamtokea kwa nia ya kumuua Joram.
Vitabu vingine ni pamoja na Zawadi ya ushindi, Tutarudi na Roho zetu, Mikononi mwa Nunda, Najiskia kuua tena, Dimbwi la damu, Roho ya paka, Pesa zako zinanuka na Malaika wa shetani.
Vitabu vinapatikana kwa bei ya shilingi 10,000 kwa kimoja kasoro Kiguu na njia kinachopatikana kwa 15,000.
Vitabu vyote vinapatika KInondoni nyuma ya jengo la airtel, Posta mkabala na sanamu la askari na BunjuA.
kwa mawasiliano tupigie simu namba 0712504985 au 0763044459.
KARIBUNI.