Vita ya DR Congo na M23 ni tafsiri ya namna watu weusi ni wabaguzi wao kwa wao, wakabila, wabinafsi n. k

strongest

JF-Expert Member
Nov 28, 2024
332
1,498
Umewhi kujiuliza kwenye hio vita ya congo ingekua ni jamii mbili tofauti ndo zinazopiganna yani mfano jamii moja iwe mtu mweus nyingine iwe mzungu au mwarabu mu asia n.k

Si kwa chuki, si kwa uchochezi, bali kwa kusema ukweli! unawezaje kumbagua mwafrika mwenzako mweusi mwenzako kisa kabila au asili yake

Vita inayoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo si vita ya kawaida—ni ni ukabila na ubaguzi wa wazi dhidi ya Watutsi.

Kwa miaka mingi, Watutsi wamekuwa wakibaguliwa, wakiteswa, na hata kulengwa kwa sababu ya utambulisho wao. Wanaitwa wageni katika nchi yao wenyewe! Wanafanywa kuwa wakimbizi wasiojulikana hatima yao!

Jamii ya kimataifa inashuhudia, lakini haichukui hatua stahiki. Serikali ya Kongo inatumia lugha ya chuki, ikiwachochea raia wake dhidi ya jamii fulani, badala ya kuleta amani na mshikamano wa kitaifa. Hii si haki!

Binafsi naona Amani haitapatikana kwa kuwabagua watu kwa kabila lao! Kila Mkongo ana haki ya kuishi kwa heshima na usalama bila kujali ukoo wake. Vita dhidi ya M23 ni kisingizio cha sera za kibaguzi dhidi ya Watutsi, na hili lazima lisemwe wazi

Hawa m23 wamenyooka wao wanachodai ni haki sawa kama raia wengine ,

Mfano rahisi Nyerere aliwahi sema huwezi kusema wamasai wa Tanzania sio raia wa Tanzania kwa sababu wanapatikana na kenya

Sisi Tanzania ashukuriwe Mungu na Nyerere hakuna ukabila
 
Back
Top Bottom