Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,855
- 34,314
Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, Rais wa Marekani Joe Biden ametoa matamshi kadhaa ambayo yameonyesha kuongeza joto uhusiano kati ya Marekani na Urusi.
Hata hivyo, maneno yake ya mwisho katika ya hotuba inayotajwa kama "hotuba kubwa" nchini Poland siku ya Jumamosi - yanaoonekana kumtaka Rais Vladimir Putin kuondolewe madarakani - inaweza kuwa suala gumu zaidi.
Katika hotuba yake mbele ya maafisa wa serikali wa Poland na waheshimiwa katika Kasri la Royal kifalme huko Warsaw, Rais wa Marekani kwa mara nyingine alionya kwamba ulimwengu uko katikati nyakati za mgogoro kati ya demokrasia na tawala za kimabavu.
Aliahidi kuwa Nato italinda "kila inchi" ya ardhi ya nchi wanachama wake. Pia aliahidi kuendelea kuiunga mkono Ukraine, ingawa alibainisha kuwa jeshi la Marekani halitaingia kupamba na na vikosi vya Urusi nchini humo.
Ilikuwa hotuba ya mashambulizi, kwa kiwango chake, iliendana na kile ambacho maafisa wa Marekani, kuanzia Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken chini, wamekuwa wakisema kwa miezi kadhaa sasa.
Kisha, kabla ya kumaliza kwa kusema "asante" na kuaga "kwaheri", Bwana Biden aliongeza kuhusu rais mwenzake huyo wa Urusi: "Kwa mapenzi ya Mungu, mtu huyu hawezi kubaki madarakani."
"Hotuba hii - na vifungu vinavyoihusu Urusi - kwa kutumia maneno ya heshima naweza sema ni vya kushangaza," msemaji wa Urusi Dmitry Peskov alisema. "Haelewi kwamba dunia sio tu Marekani na Ulaya."
"Hoja ya rais ni kwamba Putin hawezi kuruhusiwa kutumia nguvu ya madaraka juu ya majirani zake au eneo hilo," afisa wa utawala wa Biden alisema. "Hakuwa akijadili nguvu za Putin nchini Urusi, au mabadiliko ya utawala."
Mapema siku hiyo, rais wa Marekani alikuwa amemuita Putin kama "muuza nyama". Wiki iliyopita, alionekana kumshutumu kiongozi huyo wa Urusi kwa uhalifu wa kivita. Katika hoja zote mbili, matamshi ya Bwana Biden yalisababisha shutuma na onyo kutoka Moscow kwamba uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Urusi ulikuwa hatarini kuvunjika.
Rais wa Urusi Vladmir Putin
Kuna mpaka au mstari kati ya kumshutumu kiongozi wa taifa - kwa matamshi ya kidiplomasia - na kutaka aondolewe.
Mpaka huo wa matamshi uliheshimiwa sana na wamarekani na Wasovieti hata wakati wa Vita Baridi. Mpaka ama mstari ambao Bwana Biden alikuwa ameuvuka.
"Mabadiliko ya utawala" ni kitu ambacho nchi zenye nguvu zinashutumiwa kutumia kwa mataifa dhaifu - lakini sio kile ambacho taifa moja lenye silaha za nyuklia linaweza kudai kwa taifa linguine lenye nguvu na silaha hizo.
Mpaka kufikia Jumapili, wapo hata baadhi ya washirika wa Marekani waliokuwa wakijaribu kujitenga na matamshi ya Bwana Biden.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameonya kuwa rais wa Marekani anayaweka mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya Urusi na Ukraine katika hatari ya kuvunjika.
"Tunataka kuzuia vita ambavyo Urusi imeanzisha nchini Ukraine bila kuongeza zogo," alisema. "Ikiwa hicho ndico tunachotaka kukifanya, hatupaswi kuongeza mambo mengine- iwe kwa maneno au vitendo."
Mjini Washington, viongozi wa bunge pia wameelezea wasiwasi wao. Jim Risch kutoka chama cha Republican na kiongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho katika kamati ya mahusiano ya nje ya baraza la seneti, ameyaita matamshi ya Bwana Biden kuwa ni "makosa mabaya".
"Natamani wangemsaidia kubaki kwenye hotuba aliyoandaliwa," alisema. "Wakati wowote unaposema au hata, kama alivyofanya yeye, unaonyesha kuwa sera ama hoja ilikuwa ni mabadiliko ya serikali, jilo litaleta shida kubwa sana. Serikali imefanya kila wawezalo kuzuia kuongezeka.
Historia ya kusema Maneno 'bila kujitayarisha' au yasiyotarajiwa
Bwana Biden anafahamika kwa kutoa matamshi tata ya kuchochea 'vurugu' ambayo yanamuweka katika mazingira magumu. Yalivuruga jitihada zake za nyuma za kuta urais na mara kwa mara kuwavunja moyo maafisa katika utawala wa Obama wakati alipokuwa makamu wa rais. Hata hivyo, mahamshi hayo sio ya bahati mbaya. Yanaweza kufichua bayana ni wapi moyo wa Bwana Biden ulipo, hata kama kichwa chake - na vichwa vya wale walio karibu naye - kuweza kupendelea ashikilie ulimi wake.
Wakati mwingine, ni kuonyesha nguvu ya kisiasa, anaandika The Atlantic Tom Nichols, kuruhusu Bwana Biden kuungana na hisia za watu wa Marekani. Lakini, katika wakati huu wa sasa wa mgogoro wa kidiplomasia - usipochagua vizuri maneno ya kusema yanaweza kusababisha mengine - pia ni udhaifu.
"Ni vigumu kumlaumu Biden kwa kuingiza hasira zake maarufu za haraka baada ya kuzungumza na watu ambao wameteseka kutokana na ukatili wa Putin," Bwana Nichols anaandika. "Lakini maneno ya kila kiongozi wa dunia ni muhimu kwa sasa, ikiwemo hasa ya Rais wa Marekani ."
Bwana Biden anaweza kuamini kwamba uhusiano kati ya Marekani na Urusi umeharibika kiasi kwamba hauwezi ukakarabatiwa wakati Putin akiwa madarakani. Kusema wazi hivyo, hata hivyo, kunaweza kusukuma haraka lengo la Marekani - kumaliza vita nchini Ukraine huku kulinda uadilifu wa taifa - ikibaki kuwa suala gumu.
Vita nchini Ukraine haviendi kama vile Putin alivyokusudia hadi sasa. Jeshi lake limekumbwa na mapigano makali na majeruhi wanaongezeka. Uchumi wake unaporomoka kutokana na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa. Urusi inazidi kutengwa na dunia nzima.
Hali hiyo, kama kiongozi Putin wa Urusi anaona mamlaka yake yako hatarini, na ataamini kuwa Marekani haifichi hisia na kuongeza juhudi zake kwenye lengo jili, uelekeo ambao mgogoro huo unachukua kutoka tulipo huenda ukawa sio amani.
Vita vya Ukraine: Kwa nini maneno ya 'kuropoka' ya Biden kuhusu Putin ni hatari sana - BBC News Swahili
Rais wa Marekani ametoa msururu wa matamshi ambayo yameonyesha kupalia moto uhusiano kati ya Marekani na Urusi.
www.bbc.com