Vita vya kudumu Somalia sijawahi kuvielewa sababu zake, ni kama walikuwa wamechanganyikiwa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
48,153
69,517
Wakuu, hivi kuna mtu anaelewea kwa nini Somalia walipigana vita vibaya hivyo kama wendawazimu kwa miongo yote hiyo wenyewe kwa wenyewe?

Sehemu nyingi zenye vita watu wakipagana huwa sababu zinatolewa labda ni madini, mafuta, ardhi au dini lakini hawa Wasomalia hivi vyote hata hawakuwa navyo!

Ni majini yaliwapanda kichwani au kitu gani kiliwapata wakawa wanapigana vita visivyoisha?!
 
Wakuu, hivi kuna mtu anaelewea kwa nini Somalia walipigana vita vibaya hivyo kama wendawazimu kwa miongo yote hivyo wenyewe kwa wenyewe?

Sehemu nyingi zenye vita watu wakipagana huwa sababu zinatolewa labda ni madini, mafuta, ardhi au dini lakini hawa Wasomalia hivi vyote hata hawakuwa navyo!

Ni majini yaliwapanda kichwani au kitu gani kiliwapata wakawa wanapigana vita visivyoisha?!
Msomali mimi hata sielewi tunapiganiaga nini hahaha
 
Wanapigana sababu ya koo. Sio makabila maana ni kama wanafanana, tofauti ndogo ya clans zao inafanya huyu asikubali kuwa chini ya yule bora waharibikiwe wote.

Visirani na visasi ni jadi yao. Ukichanganya na Allahu akbar ndio kabisa mambo yanaharibika zaidi.
Na hukukuwahi kutokea hata clan moja yenye nguvu kuzishinda zote au yenye kuweza kuzishawishi clans nyingine zigawane madaraka zitawale kwa pamoja?
 
Awali kabisa sababu zilikuwa kushindania mamlaka. Yaani kulikuwa na vijikundi vichache vinashindania authority
Kwa nini hakukuwahi kutokea kikundi chenye nguvu kuweza kudhibiti au kushawishi wengine watulie nchi itawalike ?
 
Wanapigana sababu ya koo. Sio makabila maana ni kama wanafanana, tofauti ndogo ya clans zao inafanya huyu asikubali kuwa chini ya yule bora waharibikiwe wote.

Visirani na visasi ni jadi yao. Ukichanganya na Allahu akbar ndio kabisa mambo yanaharibika zaidi.
Yaan ww unatujua kweli, ndio hivyohivyo mbwa sisi
 
Wasomali wanachonganishwa na Waarabu.
We mbona muongo muongo sana!?..unajua kilichowakuta wamarekani walipopeleka jeshi hapo,walipeleka jeshi kufuata nini!?..unaujua umoja wa mahakama za kiislam hapo Somalia na mafanikio yao na nchi kutulia,kwa nini marekani na uingereza waliwapiga na hapajatulia mpaka leo?..jana Trump kajisifu kaua alshabaab,kinampeleka nini hapo?
 
Tueleze ukweli mwenzangu
 
Back
Top Bottom