Vita maeneo ya kazi na namna ya kuzishinda

josias

Member
Jan 7, 2014
47
34
Mara kadhaa tumekuwa tukishuhudia migogoro baina ya wafanyakazi na Watumishi wa Serikali na hata Sekta za Umma. Migogoro hiyo huambatana na , kufukuzwa kazi, kusimamishwa kazi, Kushushwa vyeo ama kutenguliwa kabisa nyadhifa za uongozi.

Nyuma ya mambo tajwa hapo juu kuna nguvu kubwa inayoitwa Vita Maeneo ya Kazi.

Kwa Ukawaida Binadamu ameumbwa na Ubinafsi (Selfishness), hivyo kwa namna yoyote ile mafanikio yako yoyote yatamuumiza na wakati mwingine atatamani nafasi yako au atatamani kukushusha hata kama hana uhakika wa Kupanda kwenda kwenye nafasi hiyo uliyo nayo.

Njia mbalimbali hutumiwa kufanikisha Vita Maeneo ya kazi. Lakin njia hizo zimegawanyika katika makundi makuu mawili:

A) Njia za Kiimani
B) Njia za Kiufundi na Kitaalamu/ Kitaalamu.

Kwenye Njia za Kiimani nako kumegawanyika katika njia kuu mbili ambazo ni Nguvu za Giza na Nguvu za Maombi.

1. Nguvu za Giza: hapa itatokana na anayekupiga Vita ana imani gani, kwa wenye imani za Nguvu za Giza wako tayari kufunga Safari maelfu ya Kilometer kutafuta namna ya Kukuangamiza. Njia hii hutumiwa na watu wenye nia mbaya maana wanajua hawawezi kutumia njia ya maombi ikafanikiwa kama wana nia mbaya na kama hauna ulilowakosea.

2. Njia ya Maombi:, Mara nyingi njia hii hutumiwa na watu wenye hofu ya Mungu na ambao wanaamini kuna namna uliwaonea ama haukuwatendea haki. Pamoja na kuwa ni njia ya Kidini, lakini hii pia ni Vita. Vita ya Wanaokuombea Mabaya utaishinda kwa Kujitetea kwa mazuri uliyowafanyia mbele za Mungu (mara zote ubaya huja baada ya Uzuri).

Njia pekee ya Kuzishinda Vita hizi mbili za Kiimani ni Kusali zaidi na Kumtegemea Mungu katika Kila jambo.

B) Vita za Kiufundi na Kitaaluma.
Kwenye Vita hizi utapigwa na watu wako wa Karibu, Wafanyakazi ama Watumishi wenzako.
Vita hizi zinaambatana na mambo yafuatayo:

i) Kukutengenezea Makosa katika Kila jambo zuri unalofanya. Watu hawa watachagua kutafuta Makosa kwenye Kila jema. Watu wa aina hii wako tayari kushikilia Doa moja lenye ukubwa wa Ncha ya Sindano kwenye Kanzu nzima, hawatothamini kuwa sehemu kubwa ya Kanzu ni safi.

ii) Jambo la Pili ni watakushauri vibaya huku wakikushangilia na ikitokea wakubwa wenu wa kazi wakahoji udhaifu fulani wao watajiweka kando na Kukuangushia zigo la lawama. (Kwenye Vita hii unaweza kusema hivi kweli hata huyu ananipiga Vita Leo)? Mara nyingi Vita hii huelekezwa kwa viongozi wa kuteuliwa na Viongozi wa Kisiasa.

Kwa Lugha nyingine wanakutengenezea ajali za kiutumishi na Kisiasa. Njia pekee ya Kushinda Vita hii ni kusimamia katiba, sheria, miongozo na kanuni kwa ukamilifu na kutumia wataalamu katika Kila jambo ili Vita hii muipigane mkiwa wanajeshi wengi.

iii) Vita nyingine ni ile ya Maadui zako kuungana na marafiki zako kwa lengo la Kukumaliza. Kwenye Vita hii usipokuwa makini kiongozi unaweza kutengenezewa Kashfa na mtu wako wa Karibu sana na ukabaki hauamini unachokiona.

Ili Kushinda Vita hii tumia Principle ya Usimuamini yeyote hata Kivuli chako mwenyewe, chukua tahadhali na unapokula na Kunywa, hata unapopita na unapolala, Hakikisha Kila unachokifanya unakifanya kwa tahadhali.

Ni vema ukifanikiwa kuwa mwajiriwa, Mchaguliwa ama Mteuliwa ukajua kuwa umeingia Vitani Rasmi. Pambana Kushinda Kila Vita iliyoko mbele yako, Kuwa makini kuchagua aina ya Wanajeshi wa kukusaidia kwenye Vita zako, kuwa makini kuchagua Silaha za Kushinda Vita zako, kubwa zaidi ya yote Mkabidhi Mungu Vita zako akupiganie.

josias
 
Back
Top Bottom