Gautten Potten
JF-Expert Member
- Aug 22, 2022
- 1,588
- 3,340
Kanisa limeweka zuio la Mkarismatic yoyote kutokuingia ndani ya Jengo
Kupishana kwao kupo wazi.
Kanisa linadai lipo sahihi kwa kile wanachosimamia na kukifuata Kama maagizo toka Ufalmeni Charismaz wanapindua order hiyo na kudai ubatili.
Asubuhi nilikuta mvutano na baadhi ya vimaswali Kama Kanisa Haliponyi Wagonjwa, Halitoi Mapepo Wala halihubiri injili ipasavyo na badala wanaenda kinyume mbona hawajioni ?
Nilipouliza zaidi mmoja akanijibu kwa swali Tata
Ndugu Trevor kwanini Wale Viziwi pale benchi la Mbele hawaponywi na badala yake wanaletewa Mtafsiri wa lugha ya Mwili na alama, Kuna Mungu hapa ?
Je, kama yupo mbona sioni maana ya ile ruhus ya kuponya vipofu, Viziwi na wengine ikitumika
ila Sisi tukitoa Mapepo na kuwaombea wagonjwa viongozi na waumini wasema Hy wapelekeeni walokole huko na wanakuja juu vibay mno
Je, Biblia inasema Nini juu ya hy tufanyayo, Ni haramu?
Sikuwa na la kujibu
Kazi kwenu.