VITA YA DAWA IANZIE BUNGENI
Bunge ni mhimili muhimu sana kwa ustawi wa Taifa. Na ni jukwaa muhimu kwa niaba ya Watanzania wote.
Ila ni mara nyingi wabunge wametuhumiwa kupokea rushwa ili kupitisha agenda zisizo na faida kwa umma au kukwamisha mambo yenye maslahi kwa umma.
Wakati wa serikali ya awamu ya tatu, kulikuwa na maambukizi makubwa ya virusi vya UKIMWI, baada ya serikali kuunda TACAIDS kampeni mubashara iliendeshwa. Na moja kama njia za kuhamasisha umma ujitokeze kupima wabunge walitakiwa kuwa mfano na kupima.
Siku ilipofika waliojitokeza walikuwa ni mawaziri pekee, wabunge karibia wote walichimba. Baadae ilitolewa ripoti ya mawaziri walio positive na negative. Ikasaidia umma nao kuhamasika kupima.
Kuna mifano mingi ya operesheni ambazo ziliharibikia bungeni sio kwa maslahi ya umma bali ya watu wachache.
Watuhumiwa wa unga kama wahalifu wengine hawatumii taratibu fulani kufanya uchafu wao bali huangalia matokeo ya wanachohitaji, suala muhimu ni kufanikisha zoezi la kuwatia nguvuni vyovyote iwezekanavyo.
Katika vita ya dawa za kulevya iliyotangazwa na RC wa DAR, Ndugu Makonda tumeona jinsi baadhi ya wabunge walivyoichukulia personal na kutetea baadhi ya washukiwa, sio wote. Hivyo ni dhahiri sio suala la utaratibu bali watu wenye maslahi nao.
Kabla ya operesheni kuna watu walilalamika na kutoa picha za waathirika, sanasana wasanii wakilaumu serikali kuwa inashindwaje kuwakamata wauzaji wakati wateja wanajulikana?
Serikali ikafanyia kazi ushauri huo, ilipowataja wasanii walewale, watu walewale waliokuwa wameibua hoja hiyo wakabeza kuwa waliotajwa ni vidagaa na wanataka mapapa.
Wanaoshukiwa ni mapapa walipotajwa sasa ndipo MAPOVU ya OMMO grade 1 yalipoanzia bungeni hadi mtaani, huku watu wakibinafsisha tuhuma au kutajwa kwa mtu na taasisi yake, kiongozi wa timu akijificha kwa wanachama wake, Mchungaji kwa waumini na wanasiasa mwavuli wa chama.
Kama mnafikiri mapapa ni furu basi mtasubiri sana, tunashindwa kujua kwamba sote ni binadamu na yote yanawezekana, na hapa ndipo unagundua kwa uwezo huu mdogo tu wa kupambanua mambo na kuishia kuwa mashabiki nchi ina safari ndefu sana kuendelea.
Nikirudi bungeni ambapo ndipo kulipaswa kutoa Mwanga na kusaidia wananchi wa kawaida nako wamekuwa kama na uwezo wa chini sana either kwa uelewa au kwa maslahi yao na watu wanaowatetea.
Njia rahisi ya kupambana na madawa, na kweli wabunge kama hawahusiki kama watumiaji au wauzaji na kwa niaba ya kusaidia watu wanaowawakilisha na kama sehemu ya vita dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya basi wapitishe azimio wabunge wote wapimwe kama wanatumia dawa za kulevya na watakaobainika wawataje wanaowauzia.
Kama sheria inavyosema, mahakama pekee ndio yenye uwezo wa kumtia mtu hatiani, nguvu kubwa ya kupinga inatia wasiwasi huenda unahusika au unawajua wahusika.
NB: WABUNGE WAWE WA KWANZA KUPIMWA, NDIO MSINGI MKUBWA WA HOJA YANGU.
Deo Meck