Visa vya matapeli na watoto wa mjini

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
283,674
737,282
Ukisikia mjini shule, shamba darasa. Jiulize hao waliotunga huo usemi walikuwa na maana gani ama walikutana na masahabu gani!

Akili ya binadamu ni kitu cha kushangaza mno. Kina uwezo wa ajabu hasa pale mtu anapokutana na changamoto mbalimbali. Huko vijijini akili nyingi zimelala kutokana na kukosa changamoto za kimaisha.

Kijijini hata kama huna kazi huna pesa utaishi tu... Sio mjini! Mjini tangu kunapambazuka mpaka kunakuchwa kila kitu ni shekeli. Hakuna cha bure mjini. Lakini vilevile mjini kila mtu anatamani kuishi maisha fulani lakini changamoto ya elimu kipato na ajira ndio kikwazo.

Hivyo basi kuweza kukabiliana na changamoto hizo watu kila uchao hubuni mbinu mpya za kuingiza kipato. Kuanzia utapeli, wizi, ujambazi, kukaba, kurubuni nknk. Kila mmoja wetu hawezi kukosa kisa cha hawa jamaa wanaoishi kwa ujanja ujanja. Nitaaza mimi kwa kusimulia vichache

Kisa cha kwanza
Huyu jamaa yeye hakuwa na kazi maalum. Ila muda wote ni msafi akionekana kama afisa fulani hivi. Siku moja akawa kakosa nauli kabisa ya kurudi nyumbani kwake Tabata na yuko kijitonyama.

Alichofanya ni kuwarubuni wale jamaa wa magari ya majitaka kuwa anataka huduma hiyo Tabata... Wakapatana bei akaenda nao mpaka mtaa wa pili kufika kwake.

Akashuka huku akiwaelekeza uchochoro mmoja kuwa ndio kwake... Akaingia hapo akatokea upande wa pili akasepa mazima....

Kisa cha pili.
Ni wale jamaa wanaorubuni watoto kuwanunulia chakula ama chochote. Ataenda na mtoto hapo mahali ataagiza kama ni bidhaa ama chakula.... Kisha atasepa na kumuacha bond mtoto wa watu..

Karibu nawe kabla sijaendelea na visa vingine

Jr
 
Mimi bingwa wa kutapeli wanaume wa mitandaoni wanitumie nauli.

Kama ni utapeli basi na mimi nipo kwenye hilo kundi najiuliza nini sababu mbna kazi ninayo pesaa ninazo lakini natapeli hela za nauli?

Basi najikuta na kesho naendelea tu kutapeli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watapeli tu maana wajinga ndio waliwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi bingwa wa kutapeli wanaume wa mitandaoni wanitumie nauli.

Kama ni utapeli basi na mimi nipo kwenye hilo kundi najiuliza nini sababu mbna kazi ninayo pesaa ninazo lakini natapeli hela za nauli?

Basi najikuta na kesho naendelea tu kutapeli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Avartar yako inaendana nawe kwa angalau asilimia 75% weka namba nami nitume nitapeliwe
 
Braza wangu anavisenti vichache mfukoni ila anataka angoe demu kwa kishua akanambie nimsindikize baa kufika kanipa mchongo kwamba dogo pesa ninazo kidogo kwahyo nikinunua kinjwaji usiwe unakunywa mpaka nikukanyage kwenye mguu. Demu katimba wakawa wanapiga story uku wanasogeza kinywaji mdogo mdogo. Mimi yangu ipo kwenye glasi ila naona bro kakausha ataki kunikanyaga kama alivyo nitonya nikamwambia bro vp mbona unakausha nikanyage basi? Utajuwa mwenyewe kilichotokea.
 
Mimi bingwa wa kutapeli wanaume wa mitandaoni wanitumie nauli.

Kama ni utapeli basi na mimi nipo kwenye hilo kundi najiuliza nini sababu mbna kazi ninayo pesaa ninazo lakini natapeli hela za nauli?

Basi najikuta na kesho naendelea tu kutapeli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Njoo unitapeli na mimi, jana nimeuza jiwe langu la dhahabu, nina milioni mia kasoro.....Labda kama sio Ngosha mimi!
 
NGOJA NIWAPE MKASA MMOJA

kuna boss wangu juzi nimemtapeli kazi aliyoniandikia pamoja na 50000 ya lodge.

Alikuwa ananitongoza nikakubali nikamwambia aniandalie document flani ambazo nilitakiwa nikaguliwe kazini kwa kuwa alijua atapata mzigo akaniandalia hizo document.

Siku ya kuzifata akaniambia yupo pale Madengo bar ya Dodoma wengi wanaifahamu. Basi nikaenda pale nikaagiza savvana kama mbili na Kitimoto rost nikazifukia nikala nikashiba.

Nikamwambia document zikwapi akasemaa hizi hapa kwenye bahasha nikazichukua nikaweka kwenye mkoba nikatulia.

Akasema tutafute lodge tukalale mm nikamwambia kwa sababu wewe ni mheshimiwa watu wakikuona itakuwa shida unatengeneza skendo nipe hela mm nikachukue chumba pale Simba hotel alafu nakupigia simu unakuja.

Akawa amenipa elfu 50000 ya chumba mm nikachukua pikpik ndruuuuki mpaka Geto kwangu.

Nilivyofik ninatumia sms usinitafute mm nipo nyumbani.

Hapa nilipo nawaza siku nikipata shida ya kikazi yeye ndiye boss wa hicho kitengo atanisaidia?

Maana alimpigia simu mpaka kiongozi wa ofisi yetu kumwambia jinsi mfanyakazi wake nilivyomtapeli.
 
Back
Top Bottom