Virusi vya udalali Tanzania

Ricky Blair

JF-Expert Member
Mar 13, 2023
456
1,002
Sidhani kama uko nyuma ilikuwa kama ivi lakini sasa inaonekana kila kona udalali wa kila kitu ingawa hata kazi ya huo udalali huioni. Kwa kawaida maana ya udalali ni kwamba anakuwa mtu wa kati ya kuwakutanisha anayetaka huduma Fulani au bidhaa na muuza bidhaa na siku zote au kwa jamii zote za kistaarabu ni muuza bidhaa au huduma ambaye anampooza dalali kutokana na makubaliano yao na haihusiani kabisa na mtaka kununua bidhaa au mnunuaji wa huduma tofauti.

Basi sasa kwa ufakara wa nchi yetu ilikuwa tu kama huruma au uungwana fulani wetu wa kijamaa kumpa mtu hela kidogo kama chenchi kama amekuelekeza mahali fulani ambapo bosi fulani yupo anauza kitu fulani na ukihofia pengine halipwi pesa nyingi kwani kama kibarua tu lakini haikuwa amri au lazima, basi sasa misukosuko mingi imeanza kuibuka na kuleta fukutu kila kona na kuanza kupigia watu kelele bila sababu kumtaka kununua kitu au achukue huduma yako kama kwa lazima na usumbufu mkubwa ingawa mtu yoyote mwenye macho anaweza kuona na kuchagua huduma au bidhaa anazotaka, mfano stendi za mabasi ya mkoani ile unatokea tu tayari umevamiwa na watu kama ishirini njoo uku unaenda Moro au Dodoma au Iringa au Mbeya wakati ofisi zote za hayo mabasi unayaona sasa sijui hapo unafanya nini Zaidi ya kumchosha mteja na kumfanya atamani hata akapandie njiani kuliko kuhangaika na kero izo, stendi ya Ubungo ilikuwa mbovu sana na hizo vitu lakini hata iyo ya Mbezi Luis nayo yale yale.

Karume pia yale yale ile hata kutoa macho tu tayari mtu ashakutupia nguo ingawa hujaomba, hii hali inakera na kuchosha san ahata mtu unajuta na unaona bora uende ukachome hela sehemu nyingine ili upate walahu ustaarabu fulani. Pia hata kama unauliza kitu fulani duka hili au lile kuna wanaojibanza kusikiliza au hata wauzaji wengine wanaruka ndio tunacho kumbe wanakimbia kwenda duka linguine iyo yote udalali kitu ambacho sio kizuri na kama huna kitu fulani unaweza ukasema sina au jaribu duka lingine. Dala dala nazo kama Boda boda yale yale ile ukiangaliana na boda boda tu tayari kashawasha pikipiki anakufuata ingawa hujampa ishara yoyote wengine hata kwenye daladala hawajashuka bado mtu kashawasha mashine anakusubiria na wengine kama kumi wapo wanakimbizana kama nyuki.

Hapo hapo izo dala dala zetu kama tunavyozijua mbovu na hazijabadilishwa Zaidi ya miaka kumi na basi moja linalotakiwa kupandisha watu ishirini na tano kistaarabu au na wengine kama watanowa kusimama limewabananisha watu hamsini nab ado debe linaendelea ingia ingia kuna siti; tutapona kweli kwa mtindo huu? Na Hapo uombee unashuka hadi mwisho kwa sababu kama ni kati kati utakoma kupenya mpaka ushuke salama kama hujaibiwa, kuchanika nguo au hata kubambiwa bila idhini yako san asana kama mwanamke au mtoto wa kike.

Watu wengi watasema iyo yote kutafuta riziki tu na sio sawa kuwalaumu kwani maisha ni magumu, Jibu langu ni moja tu na linaloeleweka ustaarabu haingalii hali ya uchumi kwani hata sokoni kuna wamama wengi wanauza nyanya, vitunguu na mbogamboga nyingi ambao wamekaa wametulia na mpaka ukiwasogelea ndo watakukaribisha muanze kufanya biashara na hata usipotamani vitu vyao unendelea kwa jirani yake na hatokuonyesha kinyongo na sio kuanza kukurukia uje kwake kama ambao madalali wengi wanafanya nje ya maduka ya bidhaa au hata migahawa ya chakula.

Pia kuna ule ustaarabu ambapo bajaji, pikipiki au daladala wanakubaliana mpaka moja lijae kwenye mstari ndo lingine linafuata na huu ustaarabu wameuanzisha wenyewe na sio kusubiri kila kitu kutoka serikali na iendelee ivyo na pia sio kupiga kelele basi ili linaenda wapi kila saa wakati kila mtu anaweza kusoma kama limeandikwa(Au labda kama linabadili ruti kama limeandikwa vingine) pia waridhike kama watu wameshajaa kistaarabu na iso mpaka tujazane kama nyuki.

Pia Boda boda wafuate ustaarabu wa kusubiri mpaka watakavyofuatwa au kuonyeshwa ishara kwamba wanahitajika kwani ukiwa na shida utafuatwa tu. Pia kwenye migahawa, maduka ya bidhaa na vitu vyote wafuate ustaarabu huo huo na kuamini kwamba watu wanaoweza kusoma au kuuliza duka la aina fulani basi kama duka lake limeandikwa duka la aina gani iwe mgahawa, duka la dawa au duka la vifaa vya ndani litaonekana tu na mtu mwenye macho ataona na haina haja ya dalali kupiga yowe kutwa nzima kama mwana injili kati kati ya mji kwa kweli inachosha na kuboa.

SUALA LA MWISHO NA LENYE KUKERA WENGI SANA IKIWEMO MIE NA KILIO CHA WATANZANIA WA KILA YA CHINI NA YA KATI NI MADALALI WA NYUMBA AU NAWEZA KUSEMA WAZI WEZI TU AU WAFIRISTI.

Hilo kundi nimeamua kuliwekea msisitizo mkali na kwa herufi kubwa kwani hawa watu wamekuwa wakisumbua sana watu nab ado wakijidai sana kwani wote tunajua serikali yetu ilivyokuwa ya kijinga na haitoweza kudili nao kama ipasavyo na Waziri wa Ardhi William Lukuvi alivyotoa amri kwamba hii tabia ya hawa madalali(Wafiristi) waache kudai hela ya mwezi mmoja kutoka kwa mpangaji na ni mwenye nyumba anayetakiwa awalipe wengi walijidai sana na hadi kutukana na kuweka posti za kejeli kwamba wanaposti nyumba ambayo sio yao kisha wanaandika kwa kejeli na dharau kwamba kama ukitaka mpigie simu Lukuvi.

Hii inaonesha ni jinsi gani hawa magaidi hawajali wanaotuumiza na wanajua iyo serikali yetu haina taaluma, dira au muda wa kudili na wao vizuri na izo amri ni amri baridi tu kama vita yao dhidi ya uchangudoa ambao unaendelea tu bila hofu yoyote.

Kwa jamii zote za kistaarabu kama nilivyosisitiza hapo mwanzo kwamba dalali ni mtu wa kawaida anayewakutanisha mnunuaji na muuzaji wa bidhaa au huduma fulani yoyote, ina maana kwa mtu yoyote mwenye akili ya kawaida hata mtoto mdogo au nyani anaelewa kwamba anayeuza ndo anatakiwa amlipe uyo dalali na sio mnunuaji kwani bila mnunuaji uyo muuzaji hapati kitu, pia dalali alipwe na muuzaji pale tu uyo muuzaji ametaka huduma yake na kampa iyo kazi na sio kwenda kujitafutia mwenyewe mteja akiwa amesikia tu juu juu fulani anauza gari au anapangisha nyumba basi anajiletea mteja bila kumuuliza uyo muuzaji.

Na pia kwa mnunuaji kama amemuambia dalali amtafutie hiyo bidhaa au huduma sawa wanaweza kukubaliana walipane vipi lakini kwa jamii yetu ya Kifiristi ambayo tunaishi kama jalala hawa watu Madalali kutwa kuposti nyumba ambazo sio zao na nyingi hata hawajepewa ruhusa na kuanza kujipangia bei, lazima walipwe service charge wengine elfu tano hawa wa mtaani na majambazi wengine wa Insta hadi elfu ishirini. Kutonesha Zaidi kidonda hawa majambazi wanakupeleka mkenge na kukutana kitu ambacho macho yako yanakusaliti kabisa na walichoposti Instagram.

Unakuta uko Insta kaposti oh nyumba ipo barabarani Mbezi beach kabisa swimming pool, gypsum, vioo vya Alluminium, Luku yako, ghorofani bla bla bla. Unafika kwanza unajikuta unapelekwa Sala sala kama sio Tegeta kabisa au Bunju na Goba. Kama hio haitoshi ndani kabisa kama mwendo wa nusu saa na pikipiki na hapo kadai barabarani au dakika mbili kwa mguu. Iyo numba ya ovyo mfereji nje unakung’ong’a na iyo ndo swimming pool yako, Luku ya kushare watu watano, madirisha ya wavu, choo cha kuchuchumaa na uongo mwingine na hapo atakupeleka nyingine kama tano za ajabu na atakuomba service charge kwa sababu kahangaika. Na mara nyingi utahangaika na kichaa mmoja utachoka utahamia mwingine utachoka kwa sababu hawajui, hawajakabidhiwa nyumba yoyote na hawawezi kuwa na uhakika wa nyumba yoyote Zaidi ya kupepesheana tu hii ipo wapi au wapi yaani wote Wafiristi tu.

Na ukiwaambia wakutumie picha ili ujue unachoenda kukutana nacho utasikia oooo sina smart phone; hela zote wanazotuibia hawana hela ya kununua hata smart phone ya elfu hamsini au sabini. Na hata kwa wale wengine wenye smart phones au iphones kabisa watakupiga chenga kutuma izo picha na hata wakituma kama izo za Insta ni za uongo, hazina taarifa kamili(mfano mtu umemuambia unataka master bedroom au iwe kwenye mtaa mzuri ila atapiga picha kuanzia mlangoni na sio nje uone papoje au atapiga chumba ambacho sio master ila atapiga picha iko chumba tofauti na choo tofauti na kujifanya ni master wakati choo kipo nje kabisa cha kushea) na cha umuhimu Zaidi hawawezi kuzizuia kuchukuliwa kwa sababu nyumba moja madalali 100 sasa ujiulize tupo kwenye jalala gani la namna hii.

Kwaiyo kwa watu wenye kipato cha chini au watu wa kati ambao wanalipwa mshahara au wanaingiza hela kwa mwezi kuanzia elfu hamsini hadi laki 8 unaweza kuona shughuli tunayokumbana nayo na hawa wafiristi, kwani utahangaika na dalali mmoja kisha akishapata service charge yake kimya utaongeza mwingine hadi unajikuta umemaliza laki moja na hamna ulichokipata na pia miundombinu mibovu na kukazania kuijenga Kinondoni tu inafanya nyumba nyingi za wilaya ya Kinondoni ziwe za ghali sana ukifananisha na Ilala au Temeka sana sana Kinondoni mwanzoni mwanzoni kama Msasani, Masaki, Mikocheni, Sinza, Kijitonyama, Mbezi Beach chini, Kinondoni au Ilala ya Posta, kariakoo au Upanga. Kuishi nje kidogo kuna changamoto kwa sababu ya usafiri na miundombinu mibovu Zaidi.

Sasa basi unaweza kuona huu ujinga unaotokea; kwani kwa jamii zilizostaarabika kwanza hao ma ajenti wa Real Estates ambao nasikia wafiristi wa huku wanaiga tu bila kuelewa maana yake. Wakala wa Real Estates uko kwa jamii zilizostaarabika ni kwamba utakuta tajiri mwenye mali nyingi au nyumba nyingi anamuachia wakala mmoja au wakala tofauti kwa nyumba izo tofauti na sio nyumba moja kuwaachia hawa chawa wetu wa mtaani na kuanza kujitangazia. Ivyo basi wakala hao wataposti izo nyumba kwa niamba ya tajiri wao na pale mteja akionekana kuvutiwa na izo atapiga simu na kuweka ahadi ya kukutana na wakala uyo na ivyo wakija kuonana hakuna cha service charge wala nini, apende asipende basi hadaiwi kitu na akipenda hatoi hela yoyote kwa dalali kwani dalali uyo analipwa na mwenye mali na sio vinginevyo. Kwaiyo mteja akitaka kupunguziwa bei au akitaka kufanya marekebisho yoyote uyo wakala ataongea na tajiri wake kujaribu kumshawishi kama akikubali au kukataa. Na pia wenye nyumba wengine sana sana wale wa uwezo wa kawaida na sio matajiri sana wana posti wenyewe na ivyo kuunganishwa na wateja wao moja kwa moja na kuua hili suala la udalali kabisa.

Hivyo ukiangalia jalala tulonalo Tanzania sana sana Dar wenye nyumba wengi sana wameonesha tama sana wakishirikiana na madalali wao bila kuogopa dhuluma wanayofanya mbele ya haki au utu wao. Utakuta linyumba la ajabu tu wala haina hata hadhi ya kumpangisha hata mbwa sembuse binadamu utasikia laki tano kwa mwezi yote tu ipo barabarani au ipo Msasani au Sinza au Makumbusho na kama iyo haitoshi miezi 6 au 10 wengine mwaka kabisa na mwezi mmoja kwenda kwa dalali. Na utakuta Dalali pia analipwa mara mbili na mwenye nyumba na mpangaji pia.

Serikali imeonekana kabisa haina uwezo na kudili na hawa mafiristi na wametamka tu ili kuonekana wanafanya kitu ingawa hawawezi kwani huu mji haujapangwa na takribani asilimia 80% watu wanaishi kwenye makazi yasiyo rasmi au yaliungana na miundombinu ya maana, ivyo basi kufuatilia kila mwenye nyumba au dalali anayofanya haya ni ngumu sana kama kufuatilia faragha ya watu wazima watakachoamua kufanya gizani.

Serikali imejaribu pia kuwakumbusha wenye nyumba walipe kodi zao kama ipasavyo kama ilivyokuwa sharia lakini kwa sababu ya changamoto nilizozitaja itakuwa ngumu sana na watawapata wale wenye mijumba ya kifahari sana ambayo sio rahisi kukimbia kodi, lakini uku mtaani sahau. Utakuta pia mteja umezunguka mwenywe kwenye baadhi ya nyumba bado mwenye nyumba anakuambia uje na dalali, Ufuska wa wapi huu? Uhuni wa wapi huu?

Yaani nimuone Idris Sultan kwenye bango anatangaza kunywa Coka niende kununua Coka niambiwe Cokae 500 lakini ongeza na mia ya kumlipa Idris Sultan? Iyo inaingia akilini? Mie ndo nilimtafuta Idris aweke tangazo au Coka ndo wamlipe Idris Sultan? Lakini hawa magaidi wote watakujibu kwa kejeli na dharau bila woga kudhani wataishi milele. Unakuta mtu kijana au binti analipwa laki tano na awahi kazini mjini na kukaa mbali kama Kimara, Bunju, Tabata au Gongo la Mboto kimbebe kwa sababu ya usafiri anajitoa mhanga kulipa laki mbili na nusu au tatu akae mjini na kajumba cha ovyo tu master bedroom ili awahi kwenda kazini bado atabinywa mwezi mzima wa dalali na miezi 6. Huu ni ukatili kabisa na nasema ipo siku mauaji yataanza kutokea na hawa dalali na wenye nyumba wa namna hii watakuwa wa kwanza na watu wakianza kushangilia msiseme sis indo wakatili, kila mtu ana mipaka yake. Hata panya akiona hana pa kwenda ukimbana atapigana tu hadi mwisho na hapo ndo anakuwa wa hatari sana.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI
Najua ni changamoto kumsajili kila mwenye nyumba ili muwajue walipe kodi lakini kitu cha kufanya hapa ni kimoja tu kwa sasa. Mtengeneze Tovuti ya serikali kubwa ambayo imlazimu kila mwenye nyumba kama kila mfanya biashara ajiandikishe na hati zake pia aziweke na kumlazimu yeye mwenyewe ndo atangaze makazi yake ili sisi tukitaka kupanga tuingie umo na kuwatoroka kabisa hao mafiristi, magaidi na majambazi wajiitayo madalali ambao wamejaa Insta kuposti picha ambazo sio hata zao.

Muwe wakali kuwaonya wenye nyumba kwamba wao ndo wa kuwalipa dalali na kama wakitaka watangaziwe kazi zao sio kazi ya mnunuaji bali ni wao ndo wa kuwalipa lakini kwa iyo tovuti itakuwa vizuri iwe inaendeshwa na mkataba pia unasainiwa na serikali inakuwa kama ndo wakala kati ya mpangaji na mwenye nyumba na pia kuwe na chaguo la chini mwezi mmoja wa kodi kwani iyo miezi 6 sisi hatulipwi mishahara ya miezi sita na muda mwingine unataka kuhama lakini iyo hela ya miezi sita unaikosa kabisa kwaiyo unataabika.

Wenye nyumba wawe wakali na kuona picha za nyumba zao zimepostiwa ovyo bila idhini wachukue hatua kali kwani ni kinyume kuchukua picha au video ya mtu au makazi ya mtu bila idhini na kuitangaza utadhani umeruhusiwa.

Sina kinyongo wala chuki na Madalali ikiwa wakielewa nini maana ya udalali ambapo ni mtu wa kati ya mnunuaji na muuzaji na akiwa anatakiwa, kama hatakiwi basi serikali ihakikishe inawaunganisha wauzaji na wanunuaji mtandaoni na kuwakwepa madalali na kama kuna wenye nyumba ambao hawatotaka kuhangaika na tovuti basi hao ndo wawaajiri hao madalali na madalali waliosajiliwa na kulipa kodi kuwatafutia wateja na hapo bado wao ndo wa kuwalipa sio sisi wapangaji.

Bila shaka mkitusaidia kwa hilo itakuwa mmetupumzisha mzigo mkubwa sana kwani tutaweza kuhama kiurahisi hata baada ya mwezi na pia kutohofia madalali au kudanganywadanganywa na pia tutakuwa na uhakika nyumba Fulani kakabidhiwa dalali Fulani ivyo ikitoka kwenye tovuti ioneshe hii imelipiwa na iwe kama dormant ivi sio hawa madalali wa Insta mtu ana post elf 3 asilimia 99% zishachukuliwa sasa unaziacha za nini?

Ni models hao? Naomba sana mtusaidie kwani tumewachoka hawa watu lasivyo mambo mabaya sana yataanza kutokea kwa sababu wametufika sana kooni, watu wengi wamedhulumiwa na wanaendelea kudhulumiwa, watu wamesainishwa mikataba feki kwa nyumba zisizokuwa zao, watu wameliwa service charge Zaidi ya laki tano ukianza kuhesabu kukutana na hao watu, watu wanaliwa hela zao za jasho na machungu kwa iyo miezi ya madalali, aisee inauma sana….Marehemu Komba aliimba MGENI AMEINGIA……MGENI MGENI MGENI UYU UKIMWI…..LAKINI MIMI NAIMBA MGENI UYU DALALI……DALALI…..DALALI…..VIRUSI VYA UDALALI.
 
Back
Top Bottom