VIPINDI VYA UMRI NA KIPATO.

Under-cover

JF-Expert Member
Nov 13, 2023
1,612
2,671
VIPINDI (4) VYA UMRI NA KIPATO KWA KILA UMRI.
.
Maisha ya mwanadamu yamegawanyika katika vipindi tofauti..
.
Wataalamu wamegawanya vipindi vya umri katika umri fulani kutegemeana na hali ya kiuchumi kwa kila kundi.
.
UMRI WA MIAKA 0_ 25

Kipindi hiki cha umri ni kipindi cha kujifunza zaidi..

Mara nyingi kipindi hiki watu huwa tegemezi na wengi wanakuwa hawana kipato cha uhakika..

Katika kipindi hiki jifunze sana elimu ya fedha, usiishie tu kupata elimu ya chuo, hakikisha unajiendeleza ili uwe na msingi mzuri wa maarifa kuhusu uchumi.
.
Watoto wako wote walio kwenye kipindi hiki hakikisha wanapata elimu ya msingi ya fedha.

UMRI WA MIAKA 26 _ 50

Huu ni umri ambao unatakiwa uwe umeshajiimarisha vizuri kiuchumi..

Usiwe unahangaika na matatizo madogo madogo, chakula na mahitaji isiwe tatizo tena kwako.
.
Umri huu hakikisha unakuwa na kazi ya uhakika, Biashara yako ilo vizuri, jenga mifumo ya uhakika ya kipato chako.

UMRI WA MIAKA 51 _ 75

Ni umri ambao unatakiwa uwe umeshatengeneza LEGACY..

Rithisha mifumo ya kutengeneza pesa kwa watu wako wa muhimu iwe ni watoto au au uliowaanda..

Rithisha watu wako vitega uchumi vyako ili viwe vinaweza kujiendesha hata bila wewe kufanya usimamizi wowote.
.
UMRI WA MIAKA 75---->

Ukifanikiwa kufikia umri huu unatakiwa hapo uwe umebakiza kumalizia siku zako..

Kwa kula chakula kizuri bila shida, Kufuata ushauri wa profeda, kukaa na wajukuu kuwapa hadhithi za maisha..
.
Na kipindi hiki kilitakiwa kianzie umri wa miaka 60 uwe umestafu na uanze kula bata..
.
Haya yote hayawezi kuja kama ulifanya makosa kwenye miaka ya 26_50

Maana hapo ndipo wengi hutengeneza maisha au kuharibu maisha..
.
Ukikosea hapo uzeeni lazima uwe mzee wa hovyo mwenye lawama na majungu..

Ukifanya vizuri utakuwa mzee mwenye hekima, busara na maokoto ya kutosha..
.
Tumia muda vizuri, ili usije kutamani siku zirudi nyuma.
.
Ukifatilia vizuri somo hili nimekulenga zaidi wewe uliye na miaka 26_50 huu ni muda wetu wa kupambana na kujenga uchumi.
.
Je umefikia kipindi gani umri? Au nikuache kwanza?
 
I can see the light at the end of the tunnel. Tuendelee kupambana
 
0 -25
26 -50
51 -75
..................
Hii ni statistics imebuniwa na mtu fulani bilashaka ni from other nations wabongo tunayo yetu!!!!
 
Back
Top Bottom