Viongozi wetu msitudanganye waziwazi

KABHILABHIGHAMBO

JF-Expert Member
Jan 15, 2017
223
113
HABARI NDUGU NA DADA WA JF

ama baada ya salaam naomba kuleta mezani kile ambacho ni maoni yangu kuhusu kile nachofikiria.

wiki nzima imepita nikiwa nafikiria sana jinsi Kesi ya Mh. Lema inavyoendeshwa na matamko ya watalaam wa sheria. Binafsi sifaham vifungu vya sheris lakini hii haininyimi nafasi ya kufikiria.

Wote tumeshuhudia watu mbalimbali wa kada mbalimbali wakitumbuliwa kwa kile kilichoitwa ni udanganyifu kwenye ofisi zao, tumewaona waalimu wakishushwa Vyeo kwa sababu mbalimbali kama vile shule zao wanazoziongoza kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa.

wiki moja iliyopita tumesikia Majaji wa mahakama ya Rufani wakitamka waziwazi kuwa DPP ameinajisi sheria, ni kusema ametenda hvyo kw makusudi na wkaongeza kwamba ofisi ya DPP wasiwafanye wao kuwa ni wa jinga. Swali langu nalojiuliza kama mahakama inasema kuwa DPP ameinajisi sheria kwa kunyima Haki Mh. Lema je hii haimanishi kwamba DPP ameshindwa kufanya kazi yake ilivyostahili?

Swali lingine nalojiuliza hao ambao walikuwa siku zote wanasema wamefungwa mikono kutoa maamuzi ya dhamana ya lema wao wantumia sheria gani ambayo ilonesha kuwa DPP yuko sawa kwa kile alichokifanya kumnyima dhamana Mh. Lema? mimi nahisi kam kuna mchezo hapa na kama hakuna mchezo wowote basi kama ilivyouwa kwa watumishi wengine basi huyu nae awajibishwe.

wito wangu kwenu nyie watawala

Yupo Mungu wa mbinguni yeye hadanganywi kama mnawafanyia watu hivi ipo siku na nyi mtawajibishwa mbele za malaika watakatifu.

hata zamani wafalme walitenda mnayoyatenda sasa miisho yao haikuwa mizuri japo waliiambiwa waache njia zao mbaya watende haki laikni hawakukubali.

kama nyie wakuu mnanisikia basi angalieni mfalme mmmoja hapa, Daniel 4: 19-28
27 Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwa hurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.
28 Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza.

tendani haki kwa wote..anayestahili hukukmu afanyiwe hivyo.

1yohana 3:
7 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;



salaam
Ndimi Khabhilabhighambo
Mkurya original.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…