Naipuli
JF-Expert Member
- Oct 8, 2012
- 266
- 110
*VIONGOZI WANGU WA DINI YA KIISLAMU HAPA TANZANIA*
_Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh_
Hivi ni kweli kwamba hadi leo hii Waislamu wa Tanzania bado tuna muda wa kulumbana na kukufurishana kuhusiana na Mwandamo wa Mwezi, Kufuga Ndevu, Kukata Suruali n.k?
Bilashaka tuna mengi yanayotuunganisha kuliko yanayotutofautisha, kwanini tuyashikilie zaidi yale yanayotutofautisha badala ya yanayotuunganisha?
Enyi ndugu zangu Waislamu, tuweni kitu kimoja, tuijenge nchi yetu, tujenge imani yetu, tuujenge Ummah wetu, tuimarishe uchumi wetu.
Waislamu wenzangu, hivi Mna Hospitali ngapi, Universities ngapi, A'Level na O'Level schools ngapi, Primary na Nursery schools ngapi, Vyuo vya ufundi vingapi na colleges nyinginezo ngapi?
Vp hivyo vilivyopo vinatosha? Au tumetosheka ni kile chuo cha "MUM" tulichopewa?
Tuna Viwanda vingapi ambavyo tunaweza kuajiri watanzania wenzetu na kuinua Uchumi wetu.
Nikiangalia wengine wana vyote hivyo nilivyovitaja, wanalipa kodi katika nchi hii, wanahudumia jamii kwa kiasi kikubwa na wanapata sapoti kubwa kutoka serikalini kuanzia lasirimali vitu hadi lasirimali watu.
Sisi kama waislamu tuna mchango gani katika nchi hii? Vp kama nikisema tumekuwa PARASITES, tunasoma vyuo na shule zao, tunatibiwa kwenye Hospitali zao, tunafanya kazi kwenye viwanda na taasisi zao, tunakula kodi zao n.k.
Hatujiskii haya wala aibu?
Hebu tubadilikeni jamani. Tuone haya, tuone aibu, tujiskie uchungu kuona na sisi tunashindwa kushiriki kikamilifu katika kuijenga nchi yetu kiuchumi, kisiasa, kiutawala, Elimu, Afya, Mazingira n.k
Lkn pia tuone uchungu kuona tunashindwa kuihudumia jamii yetu. Tuone uchungu kuona tunashindwa kushirikiana na Serikali yetu kwa kupata misamaha mbalimbali ya kodi kama ambavyo wengine wanapata kwa huduma wanazotoa katika jamii.
Au sisi tumeridhika kupata misamaha ya kodi kwenye TENDE zinazotoka SAUDIA?
Hivi kula TENDE ya kutoka SAUDIA na kwingineko kuna IMPACT gani kwa Waislamu wa nchi hii? Hivi ni kweli kwamba Waislamu wa nchi hii wanataka TENDE ili Uislamu wao uimarike? Waislamu wanataka Uchumi imara, Afya madhubuti, Elimu bora na sahihi n.k.
Au tumeridhika tukisikia mwaka huu Masheikh wetu 10 wanapelekwa HIJA na Kiongozi fulani au Taasisi fulani?
Hivi hawa Masheikh 10 au hata 100 wakipelekwa HIJA na kurudi, kuna IMPACT GANI CHANYA kwa Waislamu wa Tanzania?
Kwanini msiimarishe Uchumi ambao utanufaisha kwa kila mwenye mahitaji, iwe HIJA, Afya, Elimu n.k?!
Viongozi wetu wa Dini, Msituvuruge!
Kila mmoja abaki na msimamo wake kwa mujibu wa ijitihadi zake alizofanya katika kutafuta Elimu ya Dini.
Suala la Khitilafu lisifanywe kuwa ni Uadui baina ya Waislamu. Hivi mmeshajiuliza mtajibu nini mbele za ALLAH baada ya kufa kwenu?
Kwanini ujione wewe ni bora kuliko mwingine?
Bilashaka hizi ni dalili za Kibri na majigambo.
Bilashaka tunajifunza kisa cha Nabii Adamu (A.S) na Ibilisi, majigambo na kibri cha Ibilisi kilimfikisha wapi.
Tujikinge na Kibri na kujiona sisi ni bora kuliko wengine.
Nawaomba sana Viongozi wetu wa Dini ya Kiislamu kwa makundi na madhehebu yote kuanzia BAKWATA na Taasisi zake, Istiqama na Taasisi zake, Ansaar na wengine ambao sitaweza kuwataja hapa;
Kaeni chini kwa pamoja,
Angalieni vipaumbele vya Waislamu wa Tanzania,
Afikianeni katika yale muhimu kwa Dini yetu, Dunia yetu na Akhera yetu.
Watumieni wasomi nanwanataaluma wenu katika kuleta maendeleo na kutimiza vipaumbele vya Waumini wenu.
Vunjeni makundi yenu ambayo yanaleta uadui baina yetu sisi Waumini huku mtaani lkn ninyi mkikutana kwenye futari Ikulu na kwingineko mnasalimiana na kucheka kama kawaida.
Huenda kuna mengi ya kusema, lkn naomba kwa leo niishie hapo. Natumai meseji itafika kwa wahusika.
...............
"Shikamaneni katika Kamba ya Mwenyezi Mungu, na wala Msifarakiane"
Nimefikisha, na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa hili.
...
*Jabir Namamba*