Uchaguzi 2025 Viongozi wanajisifu kwa ujanja wa kuiba kura, kweli taifa lina hasara sana hili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mockers

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
12,806
35,261
Viongozi wa Tanzania wana kalba ya kutamka maneno ya kuudhi na kutweza wananchi,

Huyo alietamka hivyo sijui alikua kalewa au kavimbiwa, yaani eti kiongozi unajisifu Kwa kuiba kura dunia ya leo?

Maana yake huyu mkimdai katiba mpya kamwe hawezi kuwapa ushirikiano na tafanya kila awezalo kuizui,
Sio kwamba watu hawajui kama mnaiba kura wanajua, na wanaacha tu wao wakiendelea na maisha yao.

Sasa kuwaacha mnaona sasa muwapande vichwani mnajiona mna akili wakati ukweli kuna watu nje ya mfumo mkiwapa waongoze miaka kumi mingi maendeleo yatakua ya kumwaga.

Ni hayo tu viongozi badilikeni jifunzeni ethics za uongozi msilewe madaraka, Kwa sababu sio wewe Wala chama chako ambao mtadumu milele, tendeni haki mkumbukwe kwenye vitabu vya kumbukumbu njema ya taifa letu.

Pia soma
- Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!
 
Niwape tu angalizo Wanasiasa Vijana wa Vyama vyote Wasijiamini Kupita Kiasi

Kujiamini Kupita Kiasi huzaa Kiburi na kiburi ni machukizo kwa Mungu wa Mbinguni na Wanadamu WA hapa Duniani

Nimelisema hili Kwa sababu Vijana wengi wamekengeuka

Ahsanteni Sana 😂
 
Japo mimi sio Nape/Makamba... Lakini kujiamini ni muhimu.... Ni sehemu ya maisha
 
Inatakiwa ujue nyuma ya kibri Kuna nn!!

Ingawa yote haya ni ubatili mtupu na kujilisha upepo!!
 
Kura zote wapigieni upande ule lakini mjue CCM ndiyo itakayounda serikali, alisikika mtumbuaji akitamba.
 
Lile jinga kabisa sijui hata wanaoliteua wamerogwa na nani
 
Kaongoze wewe ulete faida
 
Yaani mkuu Arovela nakuunga mkono asilimia mia200hata watoto wao wanajua kuwa baba ni mwizi Ina maana hata vyeti vyao wengi ni feki.
 
Hawajui kwamba matendo mabovu hujutia uzeeni,homa si homa hiv si hiv mradi tuu ukome!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…