Viongozi wanajiona wa Muhimu sana wamelevywa na Madaraka

Tman900

JF-Expert Member
May 30, 2017
455
1,416
Mimi sio Mwanasiasa na Wala sio mtu mwenye Jina kubwa ktk hii Nchi Yenye Watu wakuu na Waliomaalumu sana.

Nimetazama Umuhimu wa Raia ktk Hii, Nchi, nimeona Uthamani wa Raia ni mdogo sana.

Kipaumbele cha serikali kwa Raia wake juu ya Ufafanunuzi wa kinachoendelea katika Nchi kwa Miaka kadhaa juu ya swala la utekaji utekaji, Wala halitolewi ufafanuzi.

Na Kila tukio linalotokea juu ya swala utekaji Wanajitambulisha kua wao ni Polisi, Je Jeshi la Polisi Limetoa Ufafanuzi gani wa wao kutoa maelezo juu ya suala la kutekana kuhusishwa na wao polisi.

Katika Nchi yeyote Duniani Kuna kua usalama wa Taifa, Swali najiuliza kama Usalama wa Taifa wao wanalionaje hili swala la kutekana na wao wanalifafanua Vipi au wao wanalitolea malezi Gani kwa Jamii, swala la kutekana.

Je, inamaana Hawa usalama wa Taifa wameshindwa Kujua watekaji, je Hapa Kuna usalama kwa Raia au Ndo usalama upo kwa Wenye mamlaka tu na sio Raia wa kawaida.

kingine cha kujiuliza je kama Watekaji wanaendelea kua na Nguvu ya kufanya Kila Jambo, Vipi siku wakiamua kufanya watakalo kwa Taifa hili, maana yake wao ni Bora, kuliko usalama wa Taifa.

Hii ni kwa Usalama wa Taifa,
Je Kama utekaji unafanyika ktk Nchi na Usalama wa Taifa mpo kimya na Raia sasa wanaanza kubishana na polisi kwa kutokua na Imani wakiofia kua ni watekaji.

Inamaana Dhaihili shahili wananchi Hawana Imani na polisi Moja kwa Moja wanajua ni watekaji, utekaji umezalisha upotevua wa Imani kwa Raia kuliamini Jeshi la Polisi sasa wanaonekana ni watekaji.

Serikali lifanyieni kazi swala la utekaji na muje na majibu kwa wananchi Ili kurudisha Imani ya Raia kwa Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi limepoteza Imani kwa Raia wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom