Viongozi waandamizi, ni vizuri kutii mamlaka na taasisi zilizowaweka mlipo kwa heshima. Zingatieni viapo na mipaka ya kazi mlizopewa

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
18,026
20,150
Katika kitabu chake cha THE 48 LAWS OF POWER, muandishi Robert Greene ameeleza kinagaubaga tahadhari muhimu sana, mila, desturi, utamaduni na maisha ya viongozi dhidi ya mamlaka za juu yao.

amefafanua maonyo na makatazo ya maana sana kwa viongozi watawala na wasaidizi woa, juu ya namna bora ya kuongoza na kukwepa makosa yasiyo muhimu yanayoweza kuleta changamoto zisizo za lazima.

Amesisitiza kwa mifano mingi mno halisi, hatua muafaka kwa viongozi waandamizi walio chini ya mamlaka, ili kuendelea kudumu kuhudumu katika nafasi au dhamana walizoaminiwa kuzitumikia.

Ni kosa kubwa kushindana na mamlaka za juu hata kama una uwezo na elimu kubwa kiasi gani.

Nadhani kuna kujisahau pakubwa miongoni mwa waandamizi katika taasisi na mashirika mbalimbali ya wananchi, kana kwamba hawapo wenye uwezo wa kufanana au kuwazidi ninyi. na wakati mwingine mnafanya haya kwa kujua, kwa makusudi au kwasabb ya ulevi tu wa madaraka.

Yamkini kuna kuabudiana miongoni mwenu wateule, huko ndani ya taasisi zenu. kushibana huku kusiko na ulazima wala maana yoyote mnakokuonyesha mpaka kwenye vyombo vya habari, kuna walakini, kuna tia mashaka utiifu wenu, uzalendo wenu juu ya mamlaka za juu.

Hivi kulikoni watu wenye viapo vyao kisheria, kupongezana hata pale viapo vinapokua vimekoma, tena vimekomeshwa na alievitoa?

Ni ujumbe gani mnatoa kwa taasisi za uteuzi? kwamba mlikutanishwa kwaajili ya kazi, kupendana au kupongezana?

Hivi wananchi wakihitimisha kwa kusema kwamba ninyi ndio mlokua mnalipa watu fedha kudhihaki viongozi waandamizi na mamlaka za juu serikalini, watakua wanakosea?

,Mliobaki serikalini na wenye dhamana mbalimbali kwenye mashirika ya umma, na wateule wapya; nendeni mkafanye ile kazi mmeaminiwa nayo mkaifanye kwa bidii, weledi na uaminifu mkubwa kwa maslahi mapana ya waTanzania..

Kumbukeni, Taasisi zenye asili ya wivu kupindukia, haziwezi kubabaika na mistakes au blunders zako kisiasa, utabanduliwa tu.

Jihadharini sana katika utendaji wenu na mamlaka hizi, daima haziwezi kuvumilia, hazioni aibu, hazina mzaha wala haya kukuchukulia hatua na kuachana nawe, ukiendekeza kiburi, jeuri majivuno, dharau, ujuaji mwingi hali ya kua umekabidhiwa dhamana ya umma.

kuna waTanzania wengi mno wenye uwezo zaidi yako..

Ukiaminiwa, aminika basi ndugu mTanzania, overconfidence zitakuathiri mwenyewe.
4Rs theory za Dr.Samia, haikua mzaha, it was real ndrugu zango..

Mungu Ibariki Tanzania 🐒

Neema na Baraka za Mungu ziambatane na kuandamana na viongozi wote wenye nafasi ya kutumikia umma, wakiongozwa na Dr.Samia Suluhu Hassan, Rais wa JMT.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom