Viongozi wa Kijeshi Burkina Faso na Mali: "Mkiigusa Niger tu mmetangaza Vita ya Ukanda"

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,804
Burkina Faso na Mali kwa pamoja zimewaonya Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kwamba wakithubutu kuvamia Nchi ya Niger ili kuwakabili Wanajeshi waliompindua Rais wa Nchi hiyo basi itakuwa ni sawa na kutangaza vita na Nchi hizo pia na hawatosita kupigana ili kuwasaidia Wanajeshi wa Niger.

Kauli ya Burkina Faso na Mali inakuja siku moja tangu ECOWAS itishie kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya utawala wa Niger baada ya kumpindua Rais wa Nchi hiyo Wiki iliyopita ambapo ECOWAs iliwapa siku saba Wanajeshi wamrejeshe madarakani Rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum ambaye anashikiliwa mateka.

Burkina Faso na Mali ambazo pia zinatawaliwa Kijeshi baada ya mapinduzi, kwenye taarifa yao ya pamoja wamesema “Serikali zetu za mpito zinaunga mkono Waniger ambao wameamua kujikomboa wenyewe na kuchukua Mamlaka yao”

“Uvamizi wowote wa kijeshi kwa Niger itakuwa ni sawa na kutangaza vita kwa Burkina Faso na Mali pia na itapelekea machafuko ambayo yatauletea shida ukanda mzima, na hatutaki kushiriki kuiwekea vikwazo visivyo halali Niger”

==============

The military juntas in Burkina Faso and Mali have said any forcible attempt to restore President Mohamed Bazoum in neighbouring Niger will be seen as a declaration of war on them.

This follows a threat from a regional bloc that it would "take all measures" if the president was not reinstated.

Mr Bazoum is being held by Niger's coup leaders after being ousted last week.

France, the former colonial power, has now announced it is preparing to evacuate its citizens from Niger.

The region, threatened by an Islamist insurgency, has seen several coups in recent years.

Both Burkina Faso and Mali have severed ties with the West, in particular with France, and embraced new alliances with Russia.

Their warning marks a significant twist that could escalate the volatile regional situation.

The joint statement comes as Chadian President Mahamat Idris Déby has been in Niger leading mediation efforts on behalf of the West African bloc Ecowas to resolve the crisis.

In their joint statement, Burkina Faso and Mali threatened that if Ecowas intervened militarily, they would withdraw from the bloc and go to the defence of their eastern neighbour. They said such an intervention would be disastrous and destabilising.

Burkina Faso, Mali and Guinea are all currently suspended from Ecowas following coups in recent years.

Niger has been a key Western ally in the fight against jihadist extremism in the Sahel.

After Mali's military leaders chose to partner up with the Wagner Group of Russian mercenaries in 2021 instead of France's counter-terror force, Paris moved its centre of operations in the region to Niger.

On Sunday Ecowas gave the junta a week to reinstate the elected president, who has been confined to the presidential palace in the capital, Niamey.

Niger's junta has not commented on the demand, but vowed to defend the country from any "aggression" by regional or Western powers. It has accused France of planning military intervention.

France did not confirm or deny the claim.

In a statement quoted by Reuters news agency, the French foreign ministry said the only authority it recognised in Niger was President Bazoum's.

BBC
 
Naona Africa Magharibi Wanajeshi wanajaribu kusaidiana kusimika Utawala wa Kijeshi kwenye Kanda yao

Hii haina Afya kwa Demokrasia nategemea Makamu wa Rais wa Vyama vya Demokrasia Duniani mh Freeman Mbowe atakemea vikali uhuni wa hawa Wajeda wa Afrika Magharibi

Mungu wa mbinguni Ibariki Africa!

Hayo mapinduzi ya kijeshi yanatakiwa sana hata hapa nchini, maana hata CCM huingia madarakani kwa nguvu ya vyombo vya dola. Hivyo ni bora wanajeshi wachukue tu.
 
Naona Africa Magharibi Wanajeshi wanajaribu kusaidiana kusimika Utawala wa Kijeshi kwenye Kanda yao

Hii haina Afya kwa Demokrasia nategemea Makamu wa Rais wa Vyama vya Demokrasia Duniani mh Freeman Mbowe atakemea vikali uhuni wa hawa Wajeda wa Afrika Magharibi

Mungu wa mbinguni Ibariki Africa!
Huku mwambao wa Bahari Hindi hakuna huo mpango?
 
Style hiyo ya Jeshi kushika mamlaka japo kwa miaka mitatu ilitumika sana miaka ya 60 na 70.

Kwa mwenendo wa sasa wa vyama vyetu vya siasa na wanasiasa Afrika, inaweza kuwa muarobaini wa kuwaondoa wanasiasa madarakani waliojisahau na kudhani wana nguvu za kimungu.

Hapa kwetu pia tunahitaji miaka kama kumi hivi ya kupumzika haya mambo ya kisiasa, twende kijeshi ili nidhamu iliyokuwepo zamani irudi. 🤔
 
Naona Africa Magharibi Wanajeshi wanajaribu kusaidiana kusimika Utawala wa Kijeshi kwenye Kanda yao

Hii haina Afya kwa Demokrasia nategemea Makamu wa Rais wa Vyama vya Demokrasia Duniani mh Freeman Mbowe atakemea vikali uhuni wa hawa Wajeda wa Afrika Magharibi

Mungu wa mbinguni Ibariki Africa!
Kazi ya Wagner hiyo!!
 
Back
Top Bottom