Viongozi wa dini watembelea Bwawa la Nyerere

Rege

Senior Member
Jul 9, 2022
116
152
Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), limesema mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakuwa na manufaa makubwa manne ambayo ni kufua umeme, uvuvi, utalii na ufugaji.

Kauli hiyo wameitoa leo wakati wanazungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza ziara ya kutembelea mradi mradi huo utakaogharimu Sh6.5 trilioni ambao utaanza majaribio ya uzalishaji Februari mwakani huku uzalishaji kamili ukitarajiwa kuanza Juni 2024.

Mmoja wa waasisi wa CPCT, Askofu Slyvester Gamanywa, amesema Watanzania watakuwa na uhakika wa umeme mradi ukikamilika, lakini pia watapata fursa za kilimo, uvuvi na utalii ambazo zitawaongezea kipato kwa namna moja au nyingine.

Naye Waziri wa Nishati, January Makamba amesema moja ya faida za mradi huo ni ujenzi wa daraja jingine kubwa katika Mto Rufiji ambalo limeshakamilika, akisema kwa siku zijazo wananchi wanaotoka mikoa ya kusini kwenda Dodoma hawatalazimika kupitia Dar es Salaam badala yake watakatiza katika mradi huo hadi Chalinze.

“Mradi huu una faida katika sekta ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa barabara itakayoanzia maeneo Utete mkoani Pwani ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa mikoa ya kusini na Pwani. Pia mradi wa JNHPP utakuwa manufaa kwa sekta za maji kwa kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa urahisi,” amesema Waziri Makamba.
Waziri Makamba amesema Serikali pia inatekeleza miradi mingine ya kufua umeme ukiwamo wa Rusumo unaojumuisha Tanzania, Rwanda na Burundi ambao ujenzi wake upo mbioni kukamilika.


Viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri wa Nishati Januari Makamba, pale walipotembelea bwawa la kufua umeme la Mwl Nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…