Wakuu,
Kuna kitu, hii siyo bure! Hiki kilichotembea iwe ni kifinyo au kibunda itakuwa ni cha maana!
=====
Viongozi wa dini na siasa Mkoani Tanga wametoa pongezi na shukrani kwa juhudi za viongozi wa Serikali wa mkoa wa Tanga pamoja na wananchi katika kuhakikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 kufanyika kwa amani bila vurugu.
Kupata taarifa na matukio yote ya uchaguzi wa serikali za mitaa kqa kila mkoa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Tanga ambae pia ni Sheikh wa Mkoa wa Tanga Juma Luhwuchu ameeleza kwamba juhudi hizo pamoja na maombi kutoka kwa viongozi wa dini zilichangia kudumisha amani na utulivu katika uchaguzi.
Naye Mchungaji Haule Haule, Mjumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Tanga , ameongeza kuwa uwazi uliokuwepo kuanzia hatua za uandikishaji hadi kufanyika kwa uchaguzi ulisaidia kudumisha amani.
Kwa upande wa Kauli za viongozi wa vyama vya siasa wakiongozwa na Ramadhani Manyeko, Naibu Kamishna wa Chama cha NCCR Mageuzi Mkoa wa Tanga, ameeleza kuridhishwa na namna ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilivyoshirikiana na vyama vyote katika mchakato wa uandikishaji na uchaguzi.