Wenyeviti wa mitaa/vitongoji na vijiji na watendaji wa kamati katika kata mnakuwa mizigo mno kwa wapiga kura wenu. Hivi ni kwanini nguvu mnayokuwa nayo wakati mnaomba kura inaisha kabisa mkisha chaguliwa? tuwaite wazenbe, wasaliti ama hamjitambui?.
Mfano, kuna maagizo mengi sana ya serikali toka huko juu lakini yakifika huku chini kwenu, kwa wananchi wa chini yanakosa usimamizi kana kwamba hamupo.
Juzi rais alionesha mfano akawaambia nini maana ya usafi kwa vitendo tukitarajia kuanzia hapo mitaa itachukua hatua hiyo kama sehemu ya wajibu wenu lakini hajabu leo ukipita kwenye mitaa ndo utashangaa ambavyo uchafu mpya umezagaa, unajiuliza wenyeviti tuliowachagua wanasubiri tena rais awakumbushe?.
Hiyo iache, juzi tu waziri wa afya kaagiza ni marufuku kuuza matunda yaliyokatwakatwa kusaidia kupambana na kipindupindu lakini we pita barabarani uone, si ubungo, buguruni, makumbusho, kimara n.k.
Sehemu zote hizi yamejaa mananasi, machungwa n.k yaliyomenywa na yako wazi, unajiuliza watendaji wa chini kwanini mna usingizi wa kiasi hiki? Kwani nyie ni viongozi wa nini hasa? ama mnasubiri waziri aje mwenyewe kukamata? hebu timizeni wajibu wenu, madaraka matamu lakini mnatakiwa kuwajibika kwa jamii zenu pia.