Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 334
- 691
1. Teodoro Obiang Nguema Mbasogo - Miaka 44
Huyu anashikilia rekodi ya kuwa Mtawala aliyekaa muda mrefu zaidi madarakani. Ni Rais wa Equatorial Guinea ambaye ameshika madaraka tangu Agosti 1979 baada ya kumpindua Mjomba wake Francisco Macías Nguema.
Mbali na Afrika, Mbasogo anashikilia rekodi ya dunia pia kwa kukaa Ikulu kwa muda mrefu zaidi.
2. Paul Biya - Miaka 41
Amekuwa Rais wa Cameroon tangu Novemba 6, 1982. Anashika nafasi ya pili kwa kukaa madarakani kwa muda mrefu zaidi Barani Afrika, na ndiye Rais mzee zaidi duniani.
3. Denis Sassou Nguesso - Miaka 39
Ni Rais wa Jamhuri ya Congo kwa miaka 34 mfululizo lakini pia aliwahi kuwa Rais wa Taifa hilo kati ya mwaka 1979 hadi 1992 baadaye akarudi tena mwaka 1997 baada ya kumalizika kwa Mapigano ya Kiraia na kuendeleza utawala wake unaofikia miaka 39.
4. Yoweri Kaguta Museveni - Miaka 37
Unaweza kumuita Mzee au Babu, amekuwa Rais wa Uganda tangu mwaka 1986 muda unaomfanya kuwa kiongozi wa 4 aliyetawala kwa muda mrefu zaidi Afrika huku akishika nafasi ya kwanza kwa Afrika Mashariki.
Museveni aliingia madarakani Januari 1986 baada ya kushinda vita ya ndani iliyofuta utawala wa Milton Obote na makundi ya Idi Amin Dada Oumee.
5. Mfalme Mswati III - Miaka 37
Mswati III ni mtawala wa Eswatini (Zamani ilijulikana kama Swaziland), ndiye kiongozi mkuu wa Familia ya Kifalme ya Kiswazi.
Aliapishwa kuwa Mfalme Aprili 25, 1986 akiwa na miaka 18 na kumfanya kuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi duniani kwa wakati huo.
Mswati anaiongoza Eswatini akiwa na Mama yake mzazi, Ntfombi Tfwala, ambaye ndiye Mama Malkia, unaweza kumwita Ndlovukati.
6. Isaias Afwerki - Miaka 37
Huyu ni Rais wa kwanza wa Eritrea ambaye amekuwa madarakani tangu taifa hilo lilipopata Uhuru kutoka Ethiopia, Aprili 1993.
Wengine ni
7. Ismaïl Omar Guelleh, Rais wa Djibouti kwa miaka Miaka 24.
8. Mfalme Mohammed VI
Huyu ni Mtawala wa Morocco amekuwa madarakani kwa miaka 24 tangu July 1999, alipokabidhiwa Mamlaka baada ya kifo cha baba yake, Mfalme Hassan II.
9. Paul Kagame - Miaka 23
Kagame aliingia rasmi Ikulu Aprili 2000 akiwa ni Rais wa 4 wa Rwanda. Lakini amekuwa kiongozi wa taifa hilo tangu mwaka 1994 ingawa alijielekeza zaidi kwenye masuala ya Kijeshi, Mambo ya Nje na Usalama wa Nchi.
Alitwaa madaraka baada ya Rais Bizimungu kujiuzulu.