Mwaka 2015 nilifanya maamuzi ya kutafuta shamba, Mungu mwema nikapata ekari 3 na nusu. Tangia hapo mpaka leo nimehangaika na hilo shamba kulibadilisha from pori, visiki, miiba, kupishana na majoka humo na majanga mengine mengi. Nimelilima kwa maana ya kulisafisha sasa ni safi pyeeeeeeeeeeeee.
Kipindi hicho nanunua, alikuwepo rafiki yangu ambaye nilikuja kugundua baadaye kuwa japo tuna fursa wote, maana tumeajiriwa, tuna mitazamo tofauti. Yeye hakuona haja ya kujihangaisha kote huko. Anapenda maisha flani ya kufanikiwa kimishen town hivii. Baada ya kusafisha shamba, mwaka jana nikaanza ujenzi wa nyumba ndogo hapo, maana mimi siamini katika kilimo cha remote control. Nataka niishi hapo hapo, nilime na niliangalie shamba langu. Mwaka huu niko kwenye harakati za kutoboa maji chini (drill)... Mungu akipenda kabla ya April nitakuwa nimefanikisha.
Sasa jamaa yangu amenijia, anataka tulime kwa utaratibu wa ubia. Eti tuchangie gharama za kilimo(mbegu, mbolea, dawa, palizi etc). alafu tugawane mavuno ya hicho tutakachopanda (iwe ni nyanya, tikiti, vitunguu etc.). Nimemwangalia hata simmalizi yaani, natamani nimjibu nahisi naweza kumtukana. Wote tuna mishahara, na kila mmoja ana uwezo wa kuwekeza. Nimesota miaka yote minne nateketeza nguvu zangu, muda, hela na rasilimali zingine. Kuchimba maji kwa mashine ya drilling ni wastani wa 10m. nimejipinda mtu katulia tuliiii. Leo kumenoga yeye anataka kutia timu, alafu anajifanya mjuaji sana yaani kiherehere chake utadhani ndo shamba lake anavyokuja kunipangia cha kufanya. Bwege sana.
Watanzania tujifunze kujitesa kwa muda flani ili baadaye mambo yakunyookee. Ina gharama yake. Inaumiza sana watu kudanganywa na motivational speakers unasimuliwa jinsi kilimo kinavyolipa, lakini hutaki kujifikirisha pia jinsi kilimo kinavyohitaji sacrifice ya kutosha especially kipindi cha mwanzo. Unaposisimka pale unapoona mtu ana shamba la green house, au hata la nje lakini anamwagilia drip irrigation, anatoa magunia kibao ya vitunguu, nyanya au mazao mengine, unatakiwa ufikirie huyo mtu alifika fikaje hapo? Tusitake tu kuona shamba jeupe, kuna kisima cha maji, pampu na simtank alafu unasema sasa tukalime.