Vijana wanafanya kazi hawalipwi na hata chakula hawapewi, Waziri wa Nishati na Madini unalijua hilo?

tanzanite miner

JF-Expert Member
Feb 2, 2016
257
172
Unakuta mgodi umetoa na unaendelea kutoa madini kila siku lakini hakuna jiko wala mpishi. Huduma za kibinadamu hata first aid kit hakuna, ukipata ajali omba MUNGU wako ndugu zako au uwe na akiba tofauti na hivyo mauti au kilema cha maisha.

Wizara ipo na inalijua hili lakini kimya. Wizara inayohusika na ajira na usalama makazini ipo lakini shughuli zao ni kukaa maofisini na sio kutembelea maeneo walipo wafanyakazi.
Inawezakana vipi mtu akafanya kazi bila mshahara(malipo) na bila kupata chakula halafu ni mwendo wa masaa 24 ukitoka utajua unakoenda kula.

Siku hizi wanambinu moja wanatumia, madini yakitoka wafanyakazi hakuna kutoka mgodini mpaka usiku wa manane ili Wizara wasijue kama kuna production wasilipe kodi.
Waziri mhusika anzia hapo kwenye kukusanya kodi, hilo la wafanyakazi kutokulipwa na kutokupatiwa chakula najua kwenu sio big issue, basi hata hiyo mbinu ya kukwepa kodi ifuatiliwe.
 
Kamanda nn shida!? Najua unazungumzia mgodi wa kwa chusa watu kutoka usiku, huu ni utaratibu tu wa kazi, kama shifti imeenda chini saa tano usiku na ni masaa 24 , si lazima itatoka huo huo muda wa saa tano usiku ili iwe imekamilisha masaa 24!? Na kuhusu msosi, mbona watu wanakula ugali kila siku japo mboga ndo maharage tu, cha muhimu acha majungu moto ilie watu wapate rizki
 
Pelekeni malalamiko yenu tume ya usuluhishi wa migogoro ya wafanyakazi mtasadiwa. Ipo pale ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara maana mererani ipo manyara!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…