Vijana wa Dar na ajira mpya ya kubet

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,455
Wiki iliyopita nilifika hapo mjini nikitokea kwetu huku Namtumbo,
miaka kadhaa nilikuwa sijafika hapo mjini, ukweli vingi vimebadilika sana ,barabara majengo ,marefu hata usafi baaadhi ya maeneo ,lakini joto mji huo naona limezidi sana

lakini kuna hili moja limenishangaza sana hapo mjini,niliona sehemu zimepambwa na watu wanaingia na kutoka ,wanawake wanaume nikataka kujua kuna jambo gani hasa linawalowashugulisha vijana wenzangu?Dah kumbe vijana wanaingia kucheza kamari wao wanaita kubet,jamani vijana wameathirika mno na kitu hiki ,
kwa wiki moja niliyokaa hapo mjini nimegundua sehemu nyingi sana mjini hapo kumefunguliwa kamari za namna hiyo na vijana wameathirika sana na hii kitu wengi wao wamegeuza hizo ndio ajira zao za kila siku,
niwaombe vijana wenzangu hiyo sio ajira rasmi na nimchezo mbaya kabisa ambao una faida chache na hasara nyingi mno,
hebu kama maisha magumu hapo mjini njoo hata huku kuna mashamba ya korosho mengi tu tutawapa mlime .

nawasilisha bandugu
 
acha kuongea ujinga ww watu tunalisha familia kwa kutegemea betting ...mm nilianza na mtaji wa laki moja kwa mwez naingiza laki tisa ninakuwa nacheza kwa kuwapa watu 1X yaan wa nyumban ashinde au adraw au X2 yaan wa ugenini aashinde au draw sasa kwasiku unakuta unaingiza 50000 maisha yanaenda
 

nisamehe mkuu kwa ujinga wangu,ingekuwa jambo la muhimu kwa sababu umekwishaona faida yake ungechukuwa na wanao ukawafundisha ili kuongeza kipato cha family
 

mwenyewe unajiona mjanja.. "pathetic"

fanyeni kazi msitegemee kamari...
 
Ujumbe mzuri sana.. Lakini JF wana thread yao kule tena imewekwa pin kabisa ....

Wanawadumaza akili vijana wetu, inabidi serikali iangalie kwa jicho la tatu hii cancer maana ikishakomaa itakuwa ngumu kutibu
mwenyewe unajiona mjanja.. "pathetic"

fanyeni kazi msitegemee kamari...
alafu hawa ndio wanakuja kupiga kelele... pesa inashuka thamani, maisha magumu .... kumbe kazi hawafanyi uzalishaji unasimama wanashinda vijiweni kucheza kamari
sasa ninyi vijana mkae mkielewa kwamba sisi tunaobet na sisi tunakazi za kufanya mimi mwenyewe nipo kwenye shirika nimeajiliwa ninabet kama mazoea na ninabet kama napenda mpira sasa ninavyobet ninakuwa naongezea hela kama mshahara na katika kubet wapo waliokosa ajira wanabet na wapo tupo kwenye ajira tunabet katika kubet tunakaul mbiu kama zifuatazo

usibetie hela ya mkopo

betia hela ambayo hata ukiliwa hautaumia au kukuuma

bet kama fani usibet kama ajira yaan beti kama mazoeaa

na sisi wengne tunabet ila sio walev wa kunywa pombe hela zetu hatupotez kwenye ulevi bali kila siku unabet hata 4000
 
Alakini amini usiamini hawa unaowaponda hapa serekali inawatambua na wana lipa kodi, huku wewe ukiendelea kukwepa kodi kila siku.
Ndugu yangu, hakuna mlipa kodi nchi hii kuzidi TBL Lakini kulipa kodi sana haifanyi bia kuwa halali, itabaki kuwa ni pombe tu na haifai, hebu jaribu kupiga picha ya miaka 20 ijayo kwa watoto wetu au wajukuu hali itakuwaje!?
 
Ukifanya kazi unapata nini? Kamari ya kubet ni sawa na fixed akaunti. Anzeni huko ndo mje huku mtaani tunako bet

hahahaha! ati betting ni sawa na Fixed Account! .. kamari ni ulevi haina tofauti na heroin watu wanapoteza mishahara kwa ajili ya kamari...

hivi kila mtu akiwa anacheza kamari hii nchi itakwenda mbele kweli ..?! nguvu kazi itapungua no one will bother working ..
 
Ndio maana hawachezi wote. Sawa na wewe unavyofanya unayoona yanaakufaa na yanakupa faida. Usimpangie mtu matumizi ya pesa yake. Ndio maana nikakwambia ni sawa na fixed maana unaweka pesa na unaongezewa kiasi fulani bila kufanya kazi
 
watu wamepewa usia na babu zao wakati wanajiandaa kuja town then wakifika huku nao wanajifanya wanaasa watu..watu tumeongeza mitaji yetu kupitia gambling af mtu analeta pumba hapa...
 
hebu achen mambo ya ajabu nyie watu mnaosema kubet si halali.....nyie endeleen kuzini tuachen sisi tuendelea kubet
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…