OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,538
- 116,431
Vijana Njooni CCM,
View attachment 144394
Miongoni mwa sifa ambazo Chama Cha Mapinduzi kimejipambanua nazo katika Nyanja za kimataifa na kitaifa ni pamoja na utaratibu na mfumo bora wa uendeshwaji wake, kwamba ni Chama kilicho kamili katika muundo wake, misingi yake, kanuni na taratibu zake. Lakini pamoja na hayo CCM inayo historia iliyotukuka si tu ya kuikomboa TANZANIA kutoka katika mikono ya wakoloni lakini pia kusaidia mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la Sahara.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Vivaa Vijana Vivaaa !!!
uteuzi wa Makonda uliwapa ujasiri vijana!
Na uliwajengea vijana precedent ya kuwa ili ufanikiwe ni lazima usome shule na ufaulu,lakini ili ufanikiwe zaidi basi jiweke karibu na "mbuyu fulani"!
Na ndiyo maana uliona dharau ya wasiosoma dhidi ya waliosoma ikiongezeka by bounds!
"Ya nini kusoma wakati a few licks of top cats could land you a r.c or a d.c post!"
Na ndio maana kwenye utumbuaji na uhakiki wa watumishi hewa,wenye madaraka ila wenye elimu tata walihakikisha wao hawagusi,majeshi hayasumbuliwi ili tu kujilinda!
Dharau dhidi ya wasomi iliwauma watumishi wa Serikali!
Ile inferiority complex ya vihiyo wenye madaraka Serikali ilipelekea watumishi 19,000 kukosa vitumbua vyao!
Mpaka wengine wakajuta,kwanini hawakujiunga na Siasa!
Ila baada ya Anguko Kuu la Makonda,elimu imepata HESHIMA YAKE STAHIKI?
Shortcuts zimeonekana hazina faida za KUDUMU bali ni za MUDA tu!
ELIMU heshima yake imerudi!
Anaweza badilika,humu kulikuwa na watu hatari sana,siwezi kuwataja coz ni active member nitakuwa nawavunjia heshima lakini wamebadilikaUVCCM wengi hawana akili..
Matukio type kama ya Daudi Albert Bashite yataendelea sana.
Chukulia mfano wa Lizaboni unaona kuna dalili zozote za kiumbe kama huyu kubadilika..??
Kama ya Mbowe vilehv elimu ya mrisho gambo ikoje
Kooote umezunguka,ulikuwa unatafuta kwa MakondaKichwa cha habari chahusika!!
Nimebahatika kuwa karibu na vijana wa CCM katika maisha ya shule na hata maisha baada ya shule! Wengi watakubaliana nami kwamba kwa awamu ya tatu na nne vijana wengi katika chama walikuwa wakiishi maisha ya ujanja ujanja na kujikomba kwa viongozi wa ngazi za juu
Viongozi wa ngazi za juu katika chama na serikali walikuwa wanamiliki vijikundi vya vijana katika harakati zao. Nitoe mfano kidogo kwa aliyekuwa Spika wa Bunge Mh.Sita yeye walikuwa na vijana kama Nape na Makonda. Mh.Lowasa yeye walikuwa na kina Bashe,katika awamu ya nne tuliona kijana alikuja kwa kasi Mwigulu Nchemba akawanunua kina Shonza na Mtela Mwampamba.
Maisha ya namna ile yaliwafanya vijana kuwa kama watumwa wa wanasiasa,huku wakisubiri teuzi mbalimbali katika chama na serikali.
Maisha hayo yaliwafanya vijana wengine wasio karibu na viongozi hao kufanya jitihada za kujipenyeza ili angalau maisha yaweze kwenda.Wengi wa vijana hawa ni wale wasiokuwa na sifa au elimu zenye mashaka mashaka.
Sasa kwa hali iliyomkuta Mh.Makonda,je itawafanya vijana hawa kukoma kujipenyeza kwa viongozi wa CCM kwa sababu hawatakuwa na nafasi tena?na hata kama wakilindwa jamii itawaanika maovu yao?
Je ni wakati sasa kwa vijana hao kuwekeza kwenye elimu na ujasiriamali badala ya kutumia mda mwingi kujipenyeza?
Mkuu nikuulize jambo moja, na ukinijibu nitajua kweli umefanya utafiti wa kutosha. Lakini kama huna jibu waweza kusema tuu nikakusaidia (tukakusaidia) ili mada yako iende vizuri.Kichwa cha habari chahusika!!
Nimebahatika kuwa karibu na vijana wa CCM katika maisha ya shule na hata maisha baada ya shule! Wengi watakubaliana nami kwamba kwa awamu ya tatu na nne vijana wengi katika chama walikuwa wakiishi maisha ya ujanja ujanja na kujikomba kwa viongozi wa ngazi za juu
Viongozi wa ngazi za juu katika chama na serikali walikuwa wanamiliki vijikundi vya vijana katika harakati zao. Nitoe mfano kidogo kwa aliyekuwa Spika wa Bunge Mh.Sita yeye walikuwa na vijana kama Nape na Makonda. Mh.Lowasa yeye walikuwa na kina Bashe,katika awamu ya nne tuliona kijana alikuja kwa kasi Mwigulu Nchemba akawanunua kina Shonza na Mtela Mwampamba.
Maisha ya namna ile yaliwafanya vijana kuwa kama watumwa wa wanasiasa,huku wakisubiri teuzi mbalimbali katika chama na serikali.
Maisha hayo yaliwafanya vijana wengine wasio karibu na viongozi hao kufanya jitihada za kujipenyeza ili angalau maisha yaweze kwenda.Wengi wa vijana hawa ni wale wasiokuwa na sifa au elimu zenye mashaka mashaka.
Sasa kwa hali iliyomkuta Mh.Makonda,je itawafanya vijana hawa kukoma kujipenyeza kwa viongozi wa CCM kwa sababu hawatakuwa na nafasi tena?na hata kama wakilindwa jamii itawaanika maovu yao?
Je ni wakati sasa kwa vijana hao kuwekeza kwenye elimu na ujasiriamali badala ya kutumia mda mwingi kujipenyeza?
Mkuu nikuulize jambo moja, na ukinijibu nitajua kweli umefanya utafiti wa kutosha. Lakini kama huna jibu waweza kusema tuu nikakusaidia (tukakusaidia) ili mada yako iende vizuri.
Jee ni kwa nini vijana wengi hasa viongozi wa UVCCM wanatabia ya kwenda Mombasa kwa mapumziko? Nini kinapelekea tabia hiyo kushamiri kwa vijana hao?