Vugu-Vugu
JF-Expert Member
- Feb 24, 2017
- 1,344
- 1,533
Sikilizeni, Nyie vijana hasa wale mnaopata nafasi za kuongoza jaribuni kukaa mbali na matendo mabaya ya rushwa pamoja na ufisadi kuna siku majina yenu yatajadiliwa kwa mema kama ilivyo leo kwa Kafulila, Polepole, Silaa na wengine.
Leo naomba mniwie radhi kwa mada hii huenda isiwapendeze baadhi ya watu humu hasa wasiopenda kusikia Kafulila na wazalendo wengine wakitajwa na mtu yoyote kwa mema.
Lakini lazima tukubaliane kwa rekodi hizi za kizalendo zilizowekwa na Cde David Kafulila hapa Tanzania ni ngumu kuuzuia umma kumjadili iwe ni mchana au usiku hata kama tunapenda au hatupendi atajajadiliwa tu kwa merits zake hizo za kizalendo.
Binafsi kwa muda Sasa nimejipa muda wa kutosha wa kufuatilia kile kinachoandikwa humu na kuzungumzwa maeneo mbalimbali kumuhusu David Kafulila.
Nimegundua mambo makuu matatu yaliyo nyuma ya tajwa tajwa hii ya Kafulila kama ifuatavyo:-
1. Kwamba, Leo ukitenda mema au ukatenda mabaya kwa Jamii|umma taarifa zako zote zitaandikwa hewani (clouds) na Umma huo huo hata kama wewe utakuwa nje ya ulingo wa siasa au nje ya nafasi yako hiyo kama ilivyo kwa Kafulila bado umma utakujadili tu.
2.Kwamba, imefika wakati baadhi ya Watanzania hata kama wao wanapenda kupokea rushwa au kutoa rushwa bado wanafurahishwa zaidi na kiongozi anayekataa kutoa au kupokea rushwa kama ilivyo kwa huyu David Kafulila leo.
3.Kwamba, David Kafulila anapendwa na kuaminiwa zaidi na Watanzania walio wengi hasa wenye vimelea vya Hayati baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere na marais waliofuata akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan.
Pia soma
<<< Je, sifa anazopewa Kafulila zina ukweli wowote?
<<< Kwanini kila kwenye Wanasiasa 10 wa CCM wanaopendekezwa kugombea uRais David Kafulila lazima awemo?