Vijana kufanya mazoezi barabarani kiholela ni hatari

Baba GS

New Member
Nov 21, 2024
1
4
Wadau kuna mwamko mkubwa sana sasa hivi wa vijana kupenda kufanya mazoezi barabarani, tena barabara kuu kiholela🙆🏾‍♀️

Hili siyo sahihi na ikitokea bahati mbaya lori likapoteza brake maafa yatakuwa makubwa sana🙆🏾‍♀️

Ukweli ni kwamba barabara zetu zimetengenezwa kwa ajili ya vyombo vya moto na sehemu za kupita watembea kwa muguu zimeainishwa kwa mistari ya pundamilia na vibao maalum

Vijana wetu tunawapenda tuwashauri wafanye mazoezi kwenye viwanja vya public na hasa kwenye shule za umma. Ushauri hautoshi lazima wakatazwe na Serikali!

Tukilifumbia macho hili kuna siku tutashuhudia maafa makubwa sana hapa Dar kwa uzembe
 
Kwanza sio salama kiafya kukimbia kwenye tarmac road bila viatu rasmi vya kukimbilia kwenye surface ngumu.Pia ni hatari kwa wakimbiaji kutoka na muingiliano na vyombo vya usafiri.
 
Back
Top Bottom