LGE2024 Vijana Jitokezeni kwa Wingi Kujiandikisha Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa - Mbunge Tauhida Gallos Nyimbo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,470
1,162

WhatsApp Image 2024-10-12 at 20.34.10.jpeg

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi, Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo amewaomba Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Mwera kushirikiana na Viongozi wao ili waweze kuwaletea maendeleo.

Akikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo Mifuko ya Saruji na Mchanga katika Tawi la CCM Muembemchomeke, Jimbo la Mwera, Mhe. Tauhida Gallos amesema kujitokeza mashirikiano ya pamoja yatapelekea kukipatia ushindi Chama Cha Mapinduzi ifikapo uchaguzi mkuu mwaka 2025.

WhatsApp Image 2024-10-12 at 20.34.07.jpeg

Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo Amesema ili malengo yaliyopangwa na Serikali yaweze kufikiwa ikiwemo miradi ya maendeleo hakuna budi kushirikiana na kwa hali na mali kwa pande zote za viongozi na wananchi

Aidha, Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo amewaomba wananchi kuwaunga mkono Viongozi wao wakuu kwa kuyatangaza mambo mazuri wanayoyafanya ili wazidi kuwapa moyo na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.

Mbali na hayo, Mbunge Tauhida Gallos amewataka Vijana kujitokeza kwa wingi katika uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa linaloendelea ili kupata idadi kubwa ya wapiga kura na kuzidi kukipatia ushindi Chama Cha Mapinduzi ifikapo, 2025.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Jimbo la Mwera, Mhe. Mihayo Juma Nunga amesema kwa muda mrefu amewasisitiza Viongozi wa Tawi la CCM la Muembemchomeke kubuni miradi ya maendeleo ili aweze kuwaunga mkono.

Hata hivyo, Mhe. Mihayo Juma amempongeza Mbunge Tauhida Gallos kwa kukabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi na kusema utaongeza hali, mashirikiano na hamasa katika utendaji wa kazi baina ya Viongozi na Wanachama.

Nao, Wanachama wa Tawi la CCM Muembemchomeke wamesema juhudi anazozichukua kiongozi wao, Mwakilishi wa Jimbo la Mwera, Mhe. Mihayo Juma ni kubwa na kuahidi kumuunga mkono katika kutatua changamoto za Wananchi na kufikia malengo yaliyopangwa na Serikali.

WhatsApp Image 2024-10-12 at 20.34.09.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-10-12 at 20.34.04.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-12 at 20.34.04.jpeg
    518.5 KB · Views: 0
  • WhatsApp Image 2024-10-12 at 20.34.08.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-12 at 20.34.08.jpeg
    72 KB · Views: 0
  • WhatsApp Image 2024-10-13 at 18.30.26.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-13 at 18.30.26.jpeg
    70.4 KB · Views: 0
  • WhatsApp Image 2024-10-13 at 18.30.33.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-13 at 18.30.33.jpeg
    85.7 KB · Views: 0
  • WhatsApp Image 2024-10-13 at 18.30.40.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-13 at 18.30.40.jpeg
    88.5 KB · Views: 0
  • WhatsApp Image 2024-10-13 at 18.30.44.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-13 at 18.30.44.jpeg
    74.9 KB · Views: 0
CHADEMA HAWATAKI VIJANA WAJIANDIKISHE, JE WANAWAOGOPA KWENYE UCHAGUZI?

Sauti za Chadema sasa zinapaza malalamiko yasiyo na mashiko, wakidai kwamba Tume ya Uchaguzi (NEC) inaandikisha wanafunzi kwa lengo la kuwaandaa kupigia kura CCM. Ukweli ni kwamba, kila kijana mwenye miaka 18 ana haki ya kikatiba kujiandikisha na kupiga kura.

Hii siyo mbinu ya kisiasa bali ni utekelezaji wa sheria, kwani vijana waliozaliwa mwaka 2006, wakiwemo wa umri wa miaka 17 mwaka huu, watafikisha miaka 18 ifikapo mwakani. Je, Chadema wanataka kuwanyima haki zao kikatiba?

Chadema wanatakiwa kuelewa kuwa kila aliyeandikishwa ameonesha kitambulisho kinachoonesha umri wake halali. Kuibua tuhuma za "kuandikisha watoto" bila kutoa ushahidi wa vitambulisho ni mbinu ya kisiasa ya kutengeneza mazingira ya kujiondoa mapema au kutafuta kisingizio endapo watashindwa tena mwakani. Tumeona mbinu kama hizi mara kadhaa—wakishindwa, hukimbilia kusema "tulibambikiwa."

Nani anaweza kuwazuia vijana wenye ari na shauku ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi? Hili si swali la wafuasi wa CCM bali ni ishara ya hofu ndani ya Chadema, wakijua kuwa kizazi cha sasa kinatambua haki zake na hakitadanganywa kirahisi. Wanapojaribu kupinga ushiriki wa vijana, wanaonesha wazi kuwa hawataki sauti za kizazi kipya zisikike.

Kwa kifupi, malalamiko ya Chadema si hoja ya msingi bali mbinu ya kuwatisha vijana na kuwapotezea imani katika mchakato wa uchaguzi. Uchaguzi si mchezo wa kuigiza bali ni nafasi ya kila raia, awe kijana au mzee, kuamua hatma ya taifa kupitia sanduku la kura.

Kama Chadema wana hofu ya kushindwa, basi wanapaswa kujipanga na kuja na sera bora badala ya kutengeneza visingizio visivyo na msingi.
 
Back
Top Bottom