Video ya Watanzania waliotekwa Malawi yavuja, waomba msaada

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
16,266
33,880
Hii ni video ya Madereva waliotekwa na kufichwa sehemu kusiko julikana huko malawi

Iko hivi

Madereva wa malori wa Malawi (sio wa Tanzania) wana mgomo wa kutaka kuongezewa mishahara. Katika hali hiyo, hayatakiwi malori yaonekane yakipita barabarani.

Kwa hivyo wameteka malori yanayopita yote, bila kujali ni ya nchi gani. Na wagomaji wanaadhibu magari yaliyotekwa kwa mashambulizi ya mawe na nondo hivyo basi katika Mkasa huo ukawakumba watanzania wanaoendesha malori ya Kwenda Malawi!

 
Aliyeelewa atueleweshe tafadhali
Nimeelewa hivi:
Madereva wa malori wa Malawi (sio wa Tanzania) wana mgomo wa kutaka kuongezewa mishahara. Katika hali hiyo, hayatakiwi malori yaonekane yakipita barabarani.

Kwa hivyo wameteka malori yanayopita yote, bila kujali ni ya nchi gani. Na wagomaji wanaadhibu magari yaliyotekwa kwa mashambulizi ya mawe na nondo.
 
Hatuna balozi huko au kazi yake kusaini karatasi tu ofisini?
Kwa taarifa yako miaka hii ktk nchi ambayo wananchi wake wanaonewa sana huko nje(nchi za kiafrika)hasa zilizoko jilani zetu, na husikii tamko kali kutoka serikalini ni Watanzania, hasa wanafanya kazi za udreva!!wakiwa zambia, DRC, malawi, uganda, kote huko ni manyanyaso tu, wakipeleka kero zao ndipo utasikia michakato inaanza ya kuangalia sheria!

Halafu jitu lina kuja kuanza kusema ohhhh watu hawana uzalendo na nchi yao! Huo uzalendo utatoka wapi hapo, waangalie wazungu juu ya raia wao wanapokuwa kwenye matatizo, serikali zao zitajitahidi hadi hatua ya mwisho, hata wakishindwa ndugu wanaona kabisa kweli serikali ilijitahidi.
 
Back
Top Bottom