The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,547
- 3,185
Moderator JF:
1. Tafadhali usiunganishe uzi huu na mwingine. Uchambuzi huu muktadha na maudhui yake ni tofauti kabisa na chambuzi za wengine waliokwisha kupost humu akiwemo Mama Amon...........
2. Uchambuzi huu unaofanywa na mwandishi nguli wa habari za kiuchunguzi anayeishi uhamishoni Uingereza ndugu Ansbert Ngurumo, umejikita zaidi kwenye kutoa kasoro za hotuba hiyo, kumuonya Rais na pia kumshauri namna njema ya kwenda mbele. Msiogope kuruhusu watu kujadili, hakuna tatizo lolote la kisheria wala la kimaadili...........
Dondoo za uchambuzi huu + hotuba ya Rais mwenyewe:
• Hotuba ya jana kule Moshi ni ya "Ki - Polisi" iliyoandaliwa na polisi wenyewe (watuhumiwa wa kadhia ya mauaji) yanayoendelea sasa hapa nchini....
• Rais Samia mara kadhaa amebabaika ktk kusoma kwake hiyo hotuba iliyokuwa na kasoro na kujichanganya kwingi. Hii inathibitisha kuwa hakuipitia kabla ili alinganishe na "classified infos" anazopokea kila siku toka vyombo vingine ukiacha polisi.....
• Kali ya mwaka kabisa ni hili kuhusu Katibu Mkuu wake Dr. Emmanuel Nchimbi. Anasema ktk hotuba yake kuwa alitumiwa video clip ya Katibu Mkuu wake (CCM), ya "Slaa wa CHADEMA" na ya yule Yona wa Chalinze na kujiridhisha kuwa kuna mipango mibaya juu yake......
• Swali ni hili; Ina maana katibu mkuu wake Dr. Emmanuel Nchimbi (CCM) alifanya Press Conference na waandishi wa habari siku ile na kuzungumza aliyozungumza bila kwanza kushauriana na kuwasiliana na mwenyekiti wake, chama chake ili kupata ridhaa ya kuzungumza? Msikilize Rais utaelewa kuwa ana maana hiyo...!
• Rais anasema kifumbo kuwa kuna chama fulani kilifanya kikao hotel ya Ngurelo kule Arusha ili kupanga kumtoa madarakani kupitia vijana kuleta vurugu. Anasema ana taarifa zote. Bahati hakusema ni chama gani kwa jina. Kwanini unadhani? Hii kauli ni sawa na ya polisi waliyoitoa wiki moja iliyopita wao wakikilenga direct CHADEMA. Wao polisi wanasema kikao kilifanyika kwa njia ya mtandao wa "ZOOM"
##Kwa ufahamu na uelewa zaidi, mtazame na msikilize mchambuzi ktk video hiyo ya dakika takribani 27 hivi