John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Wakazi wa eneo la Old Vwawa mkoani Songwe wamekutana na kinachodaiwa kuwa ni mabaki ya binadamu katika shimo ambalo lilichimbwa maalum kwa ajili ya kusimika nguzo.
Shimo hilo lipo eneo hilo katika mradi wa kuweka nguzo za umeme kutoka Old Vwawa kwenda Msambawani mkoani hapo.
Mmoja wa mashuhuda katika eneo la tukio amesema kuwa baada ya kuchimba shimo hilo wachimbaji wakakuta vitu kadhaa walivyovitaka kuwa ni masalia ya mwili wa binadamu.
Baada ya kutafutwa leo Jumatano Machi 2, 2022 msimamizi wa mradi huo katika eneo la tukio, Nickson Albert akasema:
“Mimi ni kiongozi wa mradi kwa eneo hili, ni kweli sikuwepo wakati wanachimba hilo shimo, lakini nilipofika hapo wakasema wamekuta mifupa ya binadamu, cheni, bangili na vingine kadhaa.
“Inaonekana ni mwili wa miaka mingi lakini ajabu bado vitu vimekutwa katika mazingira ambapo havijaharibika sana.
“Mradi huu wa nguzo unatoka Old Vwawa unaenda Msambawani, hivyo vitu vilitolewa na kufikishwa kwa viongozi wa Serikali za mtaa ambao hawakutilia manani.
“Hadi sasa shimo halijafukiwa wala kuwekwa nguzo, hivyo vitu vimehifadhiwa na wachimbaji kwa kuwa hakuna jitihada zozote za mamlaka kuchukua hatua za ziada.
“Nimeshawasiliana na viongozi wangu wa juu ambao hawapo eneo la tukio, wamesema watakuja kwa ajili ya kujua kinachoendelea.”
Katika video ambayo wachimbaji wamerekodi wakati wakitoa hivyo vitu kwenye shimo wanasikika wakieleza kuwa mwili huo utakuwa ni wa mwanamke kwa kuwa wamekuta bangiri, cheni, jino na mifupa.