- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimeona kipande cha video kikimuonesha Rais wa Kenya William Ruto akiwa katika katika zoezi la upandaji miti akimtambulisha Waziri wa Mazingira Bibi Soipan Tuya kuwa alikuwa girlfriend wake.
Binafsi kauli ya Rais Ruto imenishangaza sana ukizingatia kwenye tukio hili alikuwa kaambatana na mkewe bibi Rachel Ruto.
Binafsi kauli ya Rais Ruto imenishangaza sana ukizingatia kwenye tukio hili alikuwa kaambatana na mkewe bibi Rachel Ruto.
- Tunachokijua
- William Ruto (alizaliwa Kamagut, wilaya ya Uasin Gishu, 21 Disemba 1966) ni mwanasiasa wa Kenya ambaye amekuwa rais wa tano wa nchi ya Kenya kuanzia tarehe 15 Septemba, 2022.
Soipan Tuya aliwahi kuwa katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu. Aliachishwa kazi tarehe 11 Julai 2024, kabla ya kuteuliwa kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine tena tarehe 18 Julai 2024. Hata hivyo, baadaye aliteuliwa kuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri, Wizara ya Ulinzi.
Mnmo Mei 10, 2024 Rais Ruto aliongoza kampeni ya upandaji miti nchini Kenya katika msitu wa Kiambicho kaunti ya Murang’a.
Mara baada ya zoezi hilo ilianza kusambaa video kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikimuonesha Rais Ruto akiwa anazungumza kwenye Siku hiyo ambayo aliongoza zoezi la upandji miti, huku akisikika akimtambulisha Soipan Tuya kama Waziri wa Mazingira na kuongeza kuwa aliwahi kuwa Girlfreind wake siku za nyuma. Tazama baadhi hapa, hapa, hapa, hapa na hapa.
Je, ukweli ni upi?
Jamiicheck imefuatilia tukio la tarehe Mei 10, 2024 kwa kutumia ufuatiliaji wa kimtandao la Rais Ruto kuwaongoza Wakenya kupanda miti katika msitu wa Kiambicho kaunti ya Murang’a na kubaini kuwa Rais Ruto alimtambulisha kama Girlfreind wake wa zamani ambaye ni mke wake Mama Rachel Ruto na hakumtambulisha Soipon Tuya kama Girlfriend wake wa zamani kama video inavyodai bali alimtambulisha kama Waziri wa Mazingira(Tazama video hapa)
Huyu anaitwa Mama anaitwa First Lady, Huyu anaitwa Rachel huyu alikuwa Girlfreind wangu zamani, anang'ang'a na mimi, mimi ni mtu wa shida nyingi mara nyingine ananiombea mara ananifanya nini ila ananifanyia kazi nzuri. (Ruto akimtambuisha Rachel Ruto)
Na huyu ni Wazari anaitwa Soipon Tuya, huyu msichana, mnaona kama ni msichana, ndiyo Waziri wetu wa Mazingira.(Ruto Akimtambulisha Waziri Saipon)
JamiiCheck imebaini kuwa video inayoonesha Rais Ruto akimtambulisha Soipan Tuya kama Girfriend wake wa zamani imehaririwa kwa lengo la kupotosha, kwani kuna kasoro zifutazo kwenye video hiyo:-
Kasoro zilizoko kwenye video hiyo
Sauti (maneno) haindani na namna Midomo ya Rais Ruto inaongea, inaonesha kuwahi na kuchelewa kwa baadhi ya maneno na sauti kwa baadhi ya sehemu, hii ni ishara ya kawaida ya kuchezewa kwa video.
Ubora wa Sauti: Kipande cha sauti inayomtaja Soipan Tuya kama mpenzi wa zamani wa Ruto ina sauti isiyolingana ikilinganishwa na hotuba yote, ikionyesha kuwa ilikatwa na kuungwa ungwa kutoka kwenye video ya asili na kutengenezwa. Hii pia ni ishara ya kuchezewa kwa video.