Video: Maajabu ya kisima kinachowaka katika ya maji

Hapo lazima kumejaa uchawi na matambiko ya kutisha.

Naona kushoto kuna kitu kama kiti kikubwa!. usikute wabena wanaabudu hapo.

Na wewe ulikwenda huko mtoni usiku kufanya nini?

Serikali yenye akili ingeshachunguza na kufanya documentaries mbali mbali juu ya sehemu hiyo ili kujua historia na mwelekeo wa hali hiyo kwa maisha ya sasa na baadaye ye viumbe hai katika eneo hilo.

Ama ninashangaa kwa nini hiyo sehemu haijahifadhiwa vizuri kama sehemu chache za mambo tofauti ndani ya nchi.
 
Itakuwa chini kuna natural Gas . waite watalaam waje wafanye utafiti inaweza kuwa neema ingine
 
Kaka Mi natokea Kifanya mtaa wa kibondeni kwa Mzee kindimba karibu na kwa Mtewele pale,hebu nielekeze hicho kitu kiko mtaa gani
Itengule
Mtambalala
Chahucha
Ivangalala
Mapera
Kibondeni
Luhota
kiwaga juu au kiwaga?
Au kiko mtaa gani?

Nimezaliwa pale nimekua pale nimesoma pale nimeondoka juzi tu na sijawahi kusikia wala kuona.
 
Hapo Kifanya hicho kisima kiko eneo gani...
Nami nimetumiwa nimeambiwa ipo Kifanya mkoani njombe, lakini kila nikiwauliza Kifanya Sehemu gani hawanipi jibu, Mlioko Kifanya ndio inabidi mukitafute hicho Kisima Kama kweli Kipo Kifanya hapo.
 
Hapanajiuliza maswali mengi sana :

1.Hayo maji hayapati moto?
2.Kama yanapata moto mbona majani yanaaonekana yapo Green bado.
3.Naona kama ni sehemu iliyo jengewa ngazi ya kushukia humo kwenye hicho kibwawa kina kazi gani?

Mleta mada nisaidie majibu na wengine pia wenye kiu ya kujua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…