VIDEO: Jionee jinsi wanaanga wanavyoishi katika kituo cha anga cha kimataifa

International Space Station ipo umbali kama wa km.400 kutoka dunian. Inamilikiwa na USA(NASA), Russia(OPSEK), na European(ESA).Pia Canada na Japan zinahusika kusaidia matengenezo kama vile wamiliki halali,hizo juu tatu,ndizo nchi zilizo na stations kila mtu na ya kwake wameziunganisha kwa pamoja.Washirika ambao wamewai kupeleka mtu na chombo huko ni Japan(hawana eno), China juzi juzi(hawana eneo).Canada(hawana eneo).Australia(hawana).Hawana eneo maana yake hawajapeleka stations za kufanya waishi ila wanadandia za wenzao.Kila taifa lenye station linaikalabati station yake Yeye mwenyewe,ingawa wanasaidiana.Safari zilizofanywa kwenda huko ni USA 839. Russia 257 ukijumlisha na ilipoitwa Soviet.Japan 10. China 10.Israel 1. Canada 1.Britain 2.nk. Watu waliofika huko ni 543 kwa ujumla. Kwa sasa kuna watu 6 akiwemo Muingereza Timothy Peake alieenda mwezi uliopita. Marekani Timothy Kopra na Mrusi Malenchenko ambao wapo huko kati ya hao sita, ndio maastranaut waliokaa muda mref kufanya utafit, mpaka mwezi huu wana miezi 11, na wanarudi duniani mwezi wa tatu!.
 
Safi Sana kwa ufafanuzi mheshimiwa.
 
Ilipelekwa 1998. Sehem kubwa ya gharama ni kutoka USA(90%).Ilirushwa na Russia katika Station ya Baikonur Cosmodrome Kazakistan. Ingawa sehem zingine zilipelekwa na USA na Russia. Inaitwa Space laboratory. USA inaitumia kwa utafiti sana. Duniani kuna Gravity ya 10, lakin huko gravitation ni 0. Kila kitu kinaelea huko juu kwenye Space. Dunian kila kitu kikirushwa kinarudi chini. Kwenda huko unaitaji Rocket ya kukupushi na baada ya hapo Rocket inagawanyika na kubaki Spaceship ilioifadhi watu ambayo itabidi isogee taratibu na kusakwa(docking) na Capsule za International Space Station.Changamoto kubwa ipo kwenye kudakwa kwakuwa ukikosea kulenga ina maana spaceship itaikwepa kudock na kisababisha either kugonga international space station au kwenda mbali nayo.Ajari ya docking ilitoke katika chombo cha Russia kiitwacho MIR.Kilibamiza International space station Solar panels na kuziaribu. Either Spaceship au Sehem ya International space station ikiaribika angani basi inajichochea speed na kuvutwa na gravitational force ya Dunia na kuungua.Hakuna kupumua free huko,unatumia hewa ilioifaziwa.Na Crew wote wamejifungia ndani.Unaweza toka nje kufanya space walk(kuogelea),lakin ni hatari Unaweza kwenda mbali na chombo au kuvutwa na Gravitational force ya dunia au kuungua.kila kitu ufanywa kwa umakini mkubwa,kwani kosa moja ni kifo hapo hapo.
 
sasa mbona mwezi na dunia vinavutana na gravity halafu wewe unasema huko gravity ni 0
 
Sawa! Gravitational ninayozungumzia hapa ni ya ascending and descending (kwenda juu na kurudi chini) ukipush kitu kwenye space kina endelea na motion yake hivyohivyo akichepuki wala akipindi,akishuki wala akipai, kina baki pale pale kwenye orbiting yake!. Jua na dunia kweli zinavutana lakini mvutano wao ni dhaifu na stable,kuliko wewe ukirusha jiwe juu linarudi chini ghara!. Kama kuna mtu anisaidie kuelezea zaidi hapo.
 
Je mawasiliano ya huko na huku duniani yanatumika kwa njia simu au enternet 2?
 
Je mawasiliano ya huko na huku duniani yanatumika kwa njia simu au enternet 2?
Humor kuna sehemu simu zinapatikana na kompyuta kwa hiyo nadhani vyote vyaweza kutumika.pia wanaweza kutengeza electromagnetic waves kusafirisha data ardhini kwa sababu hiko pia kinaact Kama satellite. Pia kuna machine za kugeuza mkojo kuwa maji ya kunywa zinapatikana humohumo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…