Pre GE2025 VIDEO: Innocent Bashungwa alivyomsaidia mtoto huyu kumtwisha dumu kichwani baada ya kuwakuta wakichota maji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
2,299
6,314
Wakuu

Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa, ameonyesha moyo wa huruma kwa kusaidia mtoto mdogo kumtwisha dumu la maji kichwani baada ya kumkuta akichota maji.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Tukio hilo lilitokea wakati Bashungwa alipokuwa katika pita pita zake, ambapo alikutana na watoto wakichota maji. Akiwa anawaongelesha kwa lugha yao, alijitolea kumsaidia mmoja wao kwa kumtwisha dumu hilo kichwani.

Je, ni mbinu kuelekea Uchaguzi?

Inaelekea wewe huwa huna desturi ya kusaidia watu nguvukazi maana ni kawaida kwa Watz wengi kusaidiana hasa mtu anapotaka kujitwisha kitu kizito na hata maji ukipita kisimani wamama wanakuomba au wewe mwenyewe unajiongeza (hii hazihusiani na kusaidia hela ila kumtwisha mtu mzigo kawaida)
 
Maisha haya sio mchezo tunakoelekea mtu atakuwa anatembea na machawa watasema jinsi kiongozi huyu anavyotembea au anavyopumua

Jitihada za makusudi na tahadhari zichukuliwe
 
Huyo jamaa ni attention seeker na asitegemee kupata positive energy kutokana na hizo tabia za kuwachukua watu video

Anaigiza utu angekuwa Ana utu asingemjemgea mchipuko sheli na kuwaacha wananchi wanakunywa maji machafu siangejenga hata kisima cha maji.

Ile sheli aliyomjengea mchipuko is a lot of money na hela zote anatoa serikalini
 
Duh!!!Kazi kweli kweli.
Ila mimi namkubali sana jamaa,unless kama anayofanya ni kwa ajili ya attention.
 
Wakuu

Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa, ameonyesha moyo wa huruma kwa kusaidia mtoto mdogo kumtwisha dumu la maji kichwani baada ya kumkuta akichota maji.

Tukio hilo lilitokea wakati Bashungwa alipokuwa katika pita pita zake, ambapo alikutana na watoto wakichota maji. Akiwa anawaongelesha kwa lugha yao, alijitolea kumsaidia mmoja wao kwa kumtwisha dumu hilo kichwani.

Je, ni mbinu kuelekea Uchaguzi?

Kwa hiyo umeona hiyo ya maana? Na kesho atakuja kumtwisha? Hiyo imeonyesha ilivyo shida ya maji na yeye anawasaidiaje wapigakura wake.
Kuna kitu amemuuliza kwa kirugha, kwamba anasoma na mtoto akamjibu, hasomi.
Kwa point hizo mbili tu imeonyesha shida ya elimu na maji. Kwa hali hiyo atakuwa hajui shida za watu wake. Hapo hajaongolea afya, hali barabara nk. Mnapoweka video kama hizi fikiria tafsri ya wasomaji!
 
Kwa maoni yangu: Alitakiwa abebe yeye ili kumsaidia na si kumbebesha mzigo.
Hii inaleta taswira kuwa viongozi wengi kazi yao ni kubebesha raia mizigo wao wakifikiri hayawahusu.
 
Huyo jamaa ni attention seeker na asitegemee kupata positive energy kutokana na hizo tabia za kuwachukua watu video

Anaigiza utu angekuwa Ana utu asingemjemgea mchipuko sheli na kuwaacha wananchi wanakunywa maji machafu siangejenga hata kisima cha maji.

Ile sheli aliyomjengea mchipuko is a lot of money na hela zote anatoa serikalini
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom