Video iliyonitoa machozi ya mwanadada aliyedhalilishwa lodge, hatimaye wahusika wakamatwa na polisi

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,438
4,456
Ndugu zangu,

Jana usiku kaka yangu mmoja kaniletea video iliyonifanya nisipate usingizi. Ni clip mbili za dada mmoja aliyetekwa na kuwekwa chumbani na wanaume wawili. Wamempiga picha za uchi na kumtendea tukio baya kabisa.

Yule dada analia na anajaribu kuficha sura lakini anapigwa na kuingiliwa kwa nguvu. Wanazungumza kiswahili. Wanaonesha ubakaji kwa kurekodi. Shuka la nyumba linasomeka Teth Lodge, ya BOX 63. Mahali ilipo hapaonekani vema lakini ni kama vile Wami Dakawa.

Sidhani kama huyu dada ataendelea kuishi kama binadamu wa kawaida maana kisaikolojia lazima atakuwa kaumia sana hata akibaini hii clip inasambazwa tayari. Nimeshindwa kuiweka hapa kwa kuwa inasikitisha sana. Naandika nikilengwa machozi.

Sihukumu, Mungu anisamehe lakini nadhani hawa wabakaji wanastahili adhabu kali kuliko zote tuzijuazo.

Mungu ampe nguvu huyu binti.
============

TAARIFA MPYA:
Habari njema, jamaa wote wawili waliohusika kwenye tukio hilo wamekamatwa. DCI, Waziri Kitwanga wameshakamilisha kazi.
===============

UPDATE

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametaka watuhumiwa waliombaka mwanamke eneo la Dakawa mkoani Morogoro na video yake kusambazwa wafikishwe mahakamani haraka.

Haya ndio maneno ya Waziri Ummy Mwalimu katika Akaunti yake ya Facebook:

Ndugu zangu! Nimeiona dakika chache zilizopita video ya mwanamke akidhalilishwa na wanaume wawili (mashuka yanaonyesha eneo la Tiff Lodge Wami - Dakawa). Nakemea kwa nguvu zangu zote waliofanya kitendo hiki. Ni unyama uliopitiliza. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu. Hatuwezi kuuvumilia.

Nimeshamuomba Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP wachukue hatua stahiki haraka.

Pia nawaomba sana ndugu zangu msisambaze hizo video. Hiyo ni kuendelea kumdhalilisha huyo dada. Amebakwa na pia wamerekodi hilo tukio! Hii haistahimiliki na haivumiliki. Wanawake wote na wanaume wapenda haki na maendeleo ya wanawake tukemee kwa nguvu zetu zote unyama huu.
============

UPDATE - 18 May, 2016



Watuhumiwa na tukio la ubakaji na udhalilishwaji lililofanywa na wanaume wawili dhidi ya mwanamke mmoja, ambaye alipigwa picha na kusambazwa katika mitandao ya kijamii lililotokea Dakawa, Morogoro wakifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa mkoa wa Morogoro kujibu shtaka hilo.
 
Hiyo Lodge kama itajulikana itakuwa rahisi kuanzia na hapo kwa uchunguzi kama amefungua kesi hiyo clip ni ushahidi tosha.
Mungu atampa subira na hao kama ni homeboys watajulikana tu
 
Kama raia mwema unaweza kutimiza wajibu wako kwa kuikabidhi hiyo video kwa vyombo vya usalama. Nina hakika wakiwa na dhamira wanaweza kabisa kuwapata hao watuhumiwa. Itakusaidia hata wewe kupata nafuu utakapojua sheria itachukua mkondo wake.
 
Duh!! Au watu wanaujasiri kiasi gani??? Unambakaje mtu gesti??? Walimteka wakamuingiza ndani?? Je, wahudumu hawakuona?? Huyo dada kwanini hakupiga kelele, naamini wahudumu na majirani wangetoa msaada!!!
Maswali ni mengi sana.. Isije kuwa ni kitu cha "threesome gone wrong" maana duniani hapa kuna watu wana fantasy za ajabu wanazotaka kuzitimiza!!!!

Anyways, kama ni tukio la ubakaji kweli huyo binti asaidiwe na ni vizuri msomi kama wewe mackton umeiona unaweza kuwa msaada mkubwa sana kwake!! Unaweza kuokoa uhai wa mtu hapo mkuu maana watu wengine wakipitia udhalilishaji wa aina hiyo wanapatwa na msongo unaoweza kuwasababishia hata kushawishika kuondoa maisha yao wenyewe..
 
Binadamu ni viumbe wakatili sana nimeangalia pia mauaji ya watu saba sengerema na hii unayoizungumzia japo maelezo tu yanatosha kuonyesha ni namna gani huyo dada kapitia mateso. Nishafanya sana uchuguzi na kugundua kuwa si wanawake wote wanapenda umalaya isipokuwa wengine wanajikuta wanaingia katika tabia kama hizo kwa kutendwa. Duh japo kujisifu si vizuri lkn laiti kama wanaume wangekuwa na tabia kama yangu hakika dunia ingekuwa sehemu salama. Niliangalia mauaji pia ya Kamanda Mawazo hadi leo mtu akiniuliza ni kiumbe gani katili katika sayari hii basi tamjibu ni binadamu mwenye jinsia ya kiume. Pole sana kwa kuumia. Mimi kipindi flani niliomba no za mkuu wa polisi Tanzania ili nimsaidie kuwapata wakatakata mapanga huko kwetu usukumani kwani niliwahi kumfahamu mmoja (mkuu wao) lkn sikupata msaada. Mungu rudi basi
 
habari bila ushahidi ni uzushi tu,sasa sisi tutaamini vipi

weka hiyo clip hapa wataalamu wa video editing wahifanyie analysis maana unaweza ukakuta ni Bongo muvi hiyo wanatafuta kiki kama chura na gigy money
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…