Mdau shiriki kuthibitisha Video hii inayoonesha barabara ya lami yenye mashimo yenye maji ambayo ndani yake kuna mimea iliyoota huku kukiwa na watu wanotembea kwa miguu. Je, ni halisi au imetengenezwa?
- Tunachokijua
- Akili mnemba (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.
Aidha teknolojia hii imekuwa muhimu katika kurahisisha ufanisi wa shughuli za kila siku pindi tu inapotumika kwa nia iliyo njema, lakini inapotumiwa kwa nia ovu huweza kusababisha madhara makubwa kwa watu, mathalani uwepo wa taarifa potofu unachangiwa pia na teknolojia hii ambayo watu hutumia kutengeneza na kusambaza taarifa zisizo sahihi mfano picha, sauti, na video.
Madai
Video inayoonesha barabara ya lami yenye mashimo yenye maji ambayo ndani yake kuna mimea iliyoota huku kukiwa na watu wanotembea kwa miguu. Je, ni halisi au imetengenezwa?
Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa video hiyo si halisi, bali imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba.
Aidha video hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa yanayokinzana na uhalisia ikiwemo nguzo ya umeme iliyokosa muendelezo wa waya wa umeme, Pia nguzo ya pili upande wa kushoto inakosa muunganiko halisi wa waya wa umeme.
Uwepo wa mtu anayetembea katikati ya barabara hiyo akionekana kukanyaga sehemu ya maji lakini mguu hauonekani ukiingia ndani ya maji bali ukielea juu.
Pia upande wa kulia mwa video ikiwa inaanza kucheza, mtu wa tatu kati ya waliopo karibu na nguzo kadri anavyotembea mkono wake wa kushoto unaonekana kupotea ghafla.