POTOSHI Video hii inayomuonesha Rais Donald Trump akifuatiwa na mtu mrefu isivyo kawaida

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Video hii inayomuonesha Rais Donald Trump wa Marekani akifuatiwa na mtu mrefu ni halisi au imetengenezwa?
Screenshot 2025-01-21 102613.png

 
Tunachokijua
Donald Trump alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwezi novemba 2024 na kuapishwa rasmi mnamo tarehe 20, Januari 2025. Katika hafla ya uapisho Trump alikuwa pamoja na familia yake katika ikulu ya White House, mkewe pamoja na mtoto wake Barron Trump.

Kumekuwapo kipande cha video kinachomuonesha Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na mkewe wakifuatiwa mtoto wao Barron Trump ambaye anaonekana kuwa mrefu kuliko kawaida.


Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa video hiyo imepotoshwa kwa kuondolewa picha halisi ya mtoto wa Rais Trump, Barron Trump na kuwekwa picha iliyotengenezwa ambayo kijana huyo anaonekana kuwa mrefu kuliko kawaida kiasi cha kuzidi usawa wa mlango. Tazama video halisi iliyorekodiwa upande sawa na inavyoonesha video hiyo.

Kadhalika video hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa ambayo yanathibitisha kuwa imetengenezwa. Sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na kutembea kwa kijana huyo ambapo viatu vyake vikionekana kuelea juujuu huku vikiwa na mtikisiko wa kuteleza. Pia uwepo wa kivuli cha viatu kinachokinzana na mwanga unaotoka upande wa nyuma. Video kukatika pindi kijana huyo anapoufikia mlango na kushindwa kuonesha aliingiaje ndani.

Aidha katika video halisi Rais Trump akiingia ikulu ya White House akiwa ameongozana na mkewe Melania Trump huku akifuatiwa na mtoto wake Barron Trump, wote watatu wanaonekana wakiingia mpaka ndani na urefu wa Barron ni wa kawaida kiasi cha kutokuzidi usawa wa mlango tofauti na video iliyopotoshwa.​
Sio kweli. Video hii imeditiwa. Huyo mtu mrefu ni mtoto wa Trump. Na si mrefu namna hiyo. Kujihakikishia tazama motion, shadow hapo miguuni kwake sakafuni. Ni kama anatembea hewani. Plus imekatwa punde tu alipofika kwenye kizingiti cha mlango
 
Imetengenezwa,huyo ni mwanae,japo ni mrefu lakini sio hivyo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom