Huyu msukuma ni mbunge anawakilisha chama gani? Kuna taarifa nimepata kuwa ni mbunge wa ccm; kama ni hivyo basi JPM na chama chake wana kazi kubwa kuhakikisha kuwa nchi yetu inakuwa na wabunge wenye hadhi na uwezo, na hili kulifanikisha over the long term ni lazima ccm ianzie na uchaguzi wa wabunge watakaowakilisha nchi kwenye bunge la Afrika Mashariki. Safari hii ni lazima nchi kupitia vyama vya siasa vijaribu kuteua wawakilishi wenye hadhi na uwezo watakaoendana na heshima ya nchi badala ya kuchagua watu kwa kufuata urafiki na majina lakini hawala uwezo, matokeo yake ni kuitia nchi aibu kwa tabia chafu na michango katika mijadala iliyo duni!!!