Habari!
Kama inavyo jieleza kwenye kichwa, kwenye kupitia pitia kucheck tv nikakutana na mechi live za mashindani ya mpira wa miguu ya dunia kwa chini ya miaka 20 inayo endelea huko Jamhuri ya Korea.
Nilicho kiona hadi kumpeleka kupost hapa ni kwa namna hizi mechi zinavyo amriwa na waamuzi ni imekuwa tofauti na tulivyo zoea, sababu kuna waamuzi wa kawaida uwanjani na kuna wengine ambao wako kwenye chumba maalum ambao kazi yao ni kupitia picha za video kufanya kazi yao ya uamuzi kwa kusaidiwa na picha hizo.
Hasa usaidizi wao unakuja wakati wa:
- Goli - Kama kulikuwa na tatizo wakati goli linatafutwa.
- Maamuzi ya Penati.
- Kadi nyekundu.
- Kadi kupewa mchezaji kimakosa badala ya mchezaji husika.
Hatua nzima ya maamuzi inakuja pale waamuzi wa ndani wanapokuwa kwenye sehemu yao mbele ya screen kubwa zinazo ongozwa kwa teknolojia ya kugusa kwenye kioo (touch screen) ambapo muamuzi mkuu wa katikati uomba apewe muongozo endapo anapo pata utata wa tukio fulani mchezoni huku waamuzi wa kwenye chumba wakifanya kazi hiyo na kumpa taarifa.
Muamuzi wa kati anaruhusiwa kusimamisha hata mpira kutaka kujua utata wa tukio lililopita na kupewa majibu ila asisimamishe shambulio wakati anataka kusimamisha mpira akitaka kupewa taarifa.
Sina uhakika kama ni imeamriwa hivyo kwa sasa kwenye michezo mikubwa ngazi ya timu ya taifa kwa sasa au FIFA wapo kwenye majaribu kuona kama teknolojia itafaa kwenye mpira wa miguu.
Je kwa namna mpira wetu unavyo endeshwa hapa bongo, teknolojia hii itatusaidia kiasi gani?
kutokana na utata mwingi unao jitokezaga kwenye michezo yetu hapa nchini hasa kutoka kwa maamuzi ya marefa wetu.