VIDEO:AJARI MBAYA YA KUTISHA:IMETOKEA MBANDE WILAYA YA KONGWA LEO 1/9/2024

Kama kawaida uzembe na ujinga unadhidi kumaliza maisha ya Watanzania.

Viongozi wa CCM na watumishi wa umma mjikite zaidi kutatua kero za wananchi na kuboresha maisha ya watu na sio kuwaza siasa, maisha binafsi, uchaguzi na kutawala.
Dhambi za hizi roho zitawatafuna sana na vizazi vyenu.

RIP watu wa Mungu, mmekufa kwa uzembe na ujinga wa sisi ndugu zenu tusiojali maisha ya watu zaidi kujilimbikizia Mali na kujali maisha yetu ilihali mmetupa dhamana ya kuwatumikia na kutatua kero zenu.
 
Kwa nini kwa mwaka huu ajali ni nyingi? Kuna nini?

Majibu ni mafupi sana
-Mwendo kasi
-Madereva wasiotumia sheria sahihi za barabara
-Barabara mbovu
-Hali ya hewa

Ila kudai, hoo eti majini mara Mungu anatuadhibu hizo ni porojo ambazo tukiziendekeza ajali hazitaisha kamwe.

Kama ni dhambi basi ingepaswa Ulaya na America ndo waongoze kwa ajili maana wale wako level nyingine ya ukaidi kwa Mungu
 
Ajari mbaya imetokea leo asubuhi njiani kuelekea Dodoma mjini
Majeruhi ni wengi idadi ya vifo bado hijajulikana.
Ni kati ya coaster na kimbinyiko
MUNGU awape nafuu wote walio umia
Pole yao.
Lakini ukiangalia hiyo video utagundua kwamba chanzo Cha ajali hii ni:-
1. Kukosa umakini (uzembe) kwa dereva au madereva na/au Mwendokasi.
2. Miundombinu duni ya barabara. Barabara ni nyembamba Sana ikiwa na njia mbili tu (two lanes only), moja ya kwenda na nyingine ya kurudi bila ya kuwepo kwa ukingo au tuta katikati ili kutenganisha lanes za barabara.
 
Dar to Dodoma Barabara ni hatari sana, ina magari mengi, nyembamba sana, magari mabovu, madereva vichaa vichwa vibovu wasio na Elimu yeyote ya udereva, mapolisi waliobusy na kukusanya mapato.

Suluhu pekee yakuondoa hivi vifo ni kujenga miundombinu bora, kutengeneza jamii bora, kuweka mifumo bora, kuwa na viongozi wanaojali maslahi ya umma na kujua nini maana ya utumishi wa umma.

Tusubiri sababu zilezile chanzo cha ajali ni mwendokasi na uzembe wa dereva, Serikali itagharamia mazishi na matibabu ya majeruhi, imeisha hiyo life goes on.
 
Back
Top Bottom