Viashiria wavitoavyo wanaume pale wanapokuwa na mfadhaiko wa kihisia endapo hatakwambia yeye mwenyewe

Zawadi Mkweru

Member
Jan 11, 2017
5
19
1577965431530.png


Jambo moja kwa hakika: Ukiona mwanaume yeyote unayemfahamu kwenye maisha yako analia tambua kwamba kuna jambo haliko sawa. Hii ni tofauti na kwa wanawake ambapo wakilia sio lazima kuwe na tatizo kwasababu wao hutoa machozi mara kwa mara na jambo hilo hawalionei aibu na wameshazoeleka kufanya hivyo katika jamii.

Endapo wewe ni mwanamke na una mwanaume unayempenda ni vyema ukatambua namna ya kumsaidia mwenzako kuwa wazi na hisia zake ili uweze kufahamu kinachomsibu na jinsi ya kumsaidia.

Ikiwa mwenzi wako anapitia jambo nzito na linamsumbua, haya ni baadhi ya mambo atakayofanya ili kukujulisha kuwa anapitia changamoto fulani kihisia bila kusema neno lolote kwako.......

  • Kama ni mtumiaji wa vilevi matumizi yake yataongezeka zaidi ya kawaida
Anaweza akaanza kunywa kinywaji kimoja kila wakati wa chakula au hata kunywa kwa kiwango kisichoeleweka. Pia unaweza ukamkuta anakunywa kilevi mapema kuliko kawaida, au kama alizoea kunywa akiwa na marafiki atanza tabia ya kunywa akiwa peke yake. Wakati mwingine huanza kuongea maneno kama vile '' pombe ndiyo furaha yangu au rafiki yangu wa karibu''.

  • Ongezeko la ufanyaji wa baadhi ya tabia zisizo salama
Anaweza kuongeza ulaji wa aina fulani ya vyakula tofauti na kiwango alichokuwa akila hapo awali, kupenda kuangalia sana Tv, kujifunza uvutaji wa sigara au kama ni mvutaji tayari atakuwa akivuta kwa kiwango kisicho cha kawaida. Katika hali hii endapo utajaribu kumtahadharisha kuhusu madhara ya vitu anavyovifanya ataonekana au kujibu kama mtu asiyejali kwa lolote litakalomtokea.

  • Huwa na mitazamo mingi iliyo hasi
Atazidi kuwa mkali na kuwa na mitazamo hasi mingi huku akijaribu kuificha katika maneno au kauli za utani. Wakati wote huwa ni mtu mwenye majibu ya haraka au maneno ya kejeli juu ya hali au changamoto wanazopitia watu wengine.

  • Kutabasamu/Kucheka kwake hupungua hata kama anataniana na watu
Ingawa yeye anaweza kufanya au kuongea kauli za kuchekesha watu lakini yeye anaweza asicheke wala kutabasamu. Mwanaume mwenye huzuni au mfadhaiko moyoni huwa na wakati mgumu sana katika kufurahi pamoja na wale wanaomzunguka hata kama yeye ndiye atakayechekesha watu lakini yeye anaweza asicheke.

  • Huwa na tabia ya kutokujijali/kujitunza yeye mwenyewe
Anaweza akaacha kunyoa, usafi wa nguo, kukata kucha na mambo mengine yahusuyo usafi binafsi. Wakati mwanamume anapokuwa na mfadhaiko wa kihisisa huwa haoni faida ya kuujali mwili wake kwasababu anakuwa amekosa/kupoteza tumaini kuhusu maisha.

  • Huyakuza matatizo kuliko uhalisia hata kama ni madogo
Ikiwa atasikia kuhusu shida ndogo, anaifanya iwe kubwa zaidi. Ikiwa atasikia kwamba mtu ambaye hampendi ofisini atakuwa msimamizi wa jambo fulani basi ataanza kusambaza maneno ya jinsi mtu huyo atakavyoharibu kazi. Huanza kuona ubaya wa kila jambo kabla hata jambo husika halijaanza kufanyika.

  • Huwa na hasira za karibu hata katika mambo yasiyo ya msingi
Mwanaume huyu ataanza kuwa mwepesi kukasirika hasa kama hakuwa na tabia hiyo hapo awali. Kwa jambo dogo tuanaweza akakutamkia kauli mbaya au kama mko kwenye mazungumzo atanyanyuka na kuondoka kabla ya kumaliza mazungumzo yenu. Hali hii pia humfanya ajikasirikie yeye mwenyewe hata zaidi ya atakavyokukasirikia wewe.

  • Atakuwa mzito katika kushiriki tendo la ndoa
Mfadhaiko wa kihisia utamsababishia kukosa hamu ya kushiriki kimwili na mwenza wake na hata pale mwanamke utakapojaribu kumshawishi ataonekana kuwa mtu asiye na shahuku/mhemuko ya kufanya hivyo. Hali hii ni kutokana na msongo wa mawazo anaokuwa nao katika kipindi hiki.
 
Back
Top Bottom