101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,056
- 2,208
Vatican imethibitisha marufuku iliyopo kwa waumini wa kanisa katoliki kuwa wanachama wa muungano wa Freemasons.
Waraka mpya uliotiwa saini na Papa Francis umesema mafundisho ya Kikatoliki na uanachama wa Freemason hayawezi kutangamana au hayapatani.
Barua hiyo iliyotolewa na ofisi ya mafundisho ya Vatikani ilinukuu tamko lililotolewa miaka arobaini iliyopita, likisema kwamba wakatoliki waliojiunga na chama cha freemason hawaruhusiwi kushiriki katika ekaristi takatifu.
Uamuzi huo wa hivi karibuni unaonekana kumjibu Askofu kutoka Ufilipino ambaye alionyesha wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa idadi ya Wakatoliki katika dayosisi yake wanaojiunga na vyama vya freemason.