Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 49,615
- 72,474
Mpaka leo hii China bara hakuna uwakilishi wa rasmi wa Kanisa Katoliki la Roma, shughuli zao zinafanywa na "underground church" ambalo ni kanisa la mafichoni na lisilotambuliwa na serikali ya China. Kanisa Katoliki la Taiwan ndili linalotambulika rasmi kama kanisa la China japo serikali ya China inapinga sana suala hili.
Chanzo cha haya yoto ni Mgogoro mkubwa uliozuka baada ya mapinduzi ya wakomunisti ambapo Mao Zedong aliamuru taasisi zote za kijamii China kuendeshwa kwa maelekezo ya mkono wa serikali ikiwemo serikali kuwa inachagua au kufanya vetting hadi ya viongozi wa kidini. Wakatoliki wao waliambiwa zaidi wanatakiwa kumkana Papa kama kiongozi wao mkuu.
Hili jambo Wakatoliki walilikataa kabisa wakashindwa kuelewana na serikali ya China ikapelekea serikali kuanzisha kitu kinachoitwa Umoja wa Wakatoli wazalendo/Catholic Patriotic Association (CCPA) kama mbadala wa kanisa Katoliki. Kwenye hili kanisa Katoliki la serikali la Kichina makadinali na Maaskofu wake huwa wanateuliwa kwa muongozo wa serikali na hawamtambui Papa kama kiongozi wao mkuu.
Upande mwingine Vatican wao hawalitambui kanisa Katoliki la Kichina/CCPA bali wanalitambua lile lilo mafichoni ikiwemo papa kuteua Maaskofu na makadinali wake kwa siri. Huko China kuna Maaskofu wa papa lakini huwa hawatangazwi mpaka wanakufa! Kwa wale ambao siri zinavuja na kutiwa nguvuni na Serikali ya China huwa wananyooshwa kweli magerezani au kupotea.
Papa Francis aliyefariki alijaribu kuleta maelewano na serikali ya China ikashindikana baada ya kupata upinzani mkali kutoka ndani ya kanisa kwenye.