VAT ya Utalii ni vita ya madalali dhidi ya wazalendo

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Katika kuliangalia kwa karibu hili la nchi yetu kuweka tozo ya asilimia 18 kwa baadhi ya huduma za kitalii naiona vita ya kimaslahi iliyoibuka kati ya madalali wa utalii na Serikali inayoweka msimamo unaoungwa mkono na wazalendo wa nchi hii.

Ni vita ya kupigania maslahi ya wengi dhidi ya wachache.

Haya ni mapambano muhimu katika wakati tulio nao ambapo wenye kupigania maslahi ya kiudalali wameshafanikiwa kusambaza hofu kuwa watalii wanaikimbia nchi yetu na kwamba tunaelekea kushindwa.

Kenya inayozungumzwa kuondoa kodi hiyo ni hatua ya hila na kizandiki katika ushindani na inachangiwa pia na pigo wanalolipata kutoka na ugaidi wa el shabaab na hofu yenye kuambatana nayo hususan watalii. Inasikitisha sana na hatuna budi kuwa na mshikamano na jirani zetu wa Kenya katika vita vyao dhidi ya ugaidi.

Hata hivyo, hilo haliondoi ukweli kuwa kwenye sekta ya utalii Kenya ni washindani wetu.

Kama nchi hatuwezi kubadilisha maamuzi yetu tuliojiridhisha kuwa ni sahihi kwa vile tu Kenya wameamua vingine. Hizo ni dalili za kuyumba na kutojiamini kama taifa.

Naamini, Tanzania kama nchi bado inavutia watu wengi wa dunia kuja kuitembelea kutokana na vivutio tulivyo navyo na ambavyo vingine hata mtalii aimalize Kenya yote hawezi kuviona kama si kuzunguka dunia na mwisho kuambiwa, viko Tanzania tu.

Naamini pia, kama mtalii alishaamua kutembelea Tanzania tangu Januari mwaka huu, hawezi kufuta safari yake kwa sababu ya VAT ya asilimia 18. Vinginevyo, hakuwa na dhati ya kufunga safari ya kuja Tanzania.

Isipokuwa, naamini mtalii anaweza kufuta safari yake aliyoipanga tangu Januari kwa tishio la usalama wake, hata kama ungemuahidi kumuondolea VAT na kumkaribisha airport na glasi ya bure ya juisi ya ukwaju. Hili ni tatizo kwa wengine, sisi hatuna kwa sasa na linachangia kutuuza kiutalii.

Ni rai yangu kwa Serikali, kuwa isikubali kusogea hata hatua moja kutoka msimamo wa sasa. Tuko kwenye vita na tumezidiwa na wapinzani wetu, kwa kiasi fulani kwenye propaganda.
Vinginevyo, hata kama itachukua muda, lakini haya ni mapambano sahihi na ya haki kwetu, na uwezo wa kushinda tunao.
Maggid.

 
Kama ungelijua lilivyoathiri utalii usingezungumzia kiwepesi wepesi hivyo mimi nimwandishi nimeona mpaka mifano kwelj ma tour operator wamepata cancelation nyingi sana na utalii utashuka sana Tanzania Maana Tanzania imekua Gali kupindukia usizungumze bila kufanya tafiti
 
Ndugu Maggid,

Sekta ya Utalii ni sekta ambayo inachangia pato la Taifa kuliko Gold..

Fedha nyingi za kigeni, ajira nyingi, soko la mazao ya kilimo kama mboga na matunda

Mwaka 2014 Kenya walikuwa na watalii wengi zaidi kuliko Tanzania, japo Kenya walikuwa na misuko suko mingi sana ya kiusalama (Al Shabab).

Kulingana na World Bank report, Kenya waliizidi Tanzania kwa idadi ya watalii na kiwango cha Pesa.

Tanzania ina vivutio vingi na vizuri kuliko Kenya, Je Kwa nini Kenya wanapata watalii wengi na Pesa Nyingi zaidi?

Ndugu Maggid, Acha Propaganda...come to the real facts.....Tourism is professional Sector....Bla bla za siasa hazitakiwi

Mtalii kutoka UK, German, France and USA sio kama wewe Mtanzania sukari inapanda bei tu Kesho na unakubali..

Watalii wengi ni middle class na ni wafanyakazi....wanaweka akiba miaka 2 mpaka 5.....Kwao Budget ni kitu muhimu sana.

Tourist alishafanya makubaliano/mkataba na Travel Agent au Tour Operator na kulipia safari tangu January....So kigeu geu katika biashara haitakiwi...

Mkataba kati ya Mtalii na Tour Operator/Travel Agent ni sawa na Mkataba wa Serikali na Dowans au IPTL.....kama Magid unaona ni rahisi kuvunja mkataba.....Basi Serikali ingevunja mkataba kati ya IPTL na TANESCO..

Watalii Middle class ni wengi..na wachache sana ni Matajiri.....Cha ajabu...Mtalii Tajiri analipa Park entry fee sawa na Mtalii Middle class.

Kwa sasa kuna Cancellation nyingi, na watalii wengi hawaingalii Tena Tanzania kama Destination......Tourists are choosing other destinations

Maggid na wengine msiojua Tourism, kaeni mbali.....acheni kupotosha umma....Kama hujui Tembelea hata ofisi za TATO au TTB upewe Shule...Acha kudandia gari kwa mbele.....Utaaibika...
 
you nailed down kaka safi sana
 
Maggid, Kwanza hujaelewa suala lote la VAT kwenye Tourism....Mkurupuko Mwendokasi

Tour Operators and Travel Agents wanataka serikali iheshimu mkataba kati ya Tour Operator na mteja...So serikali iheshimu watalii ambao wameshalipa...Hivyo iahirishe mpaka 2017.

Serikali inaheshimu mkataba kati ya makampuni ya Gold....Au Mkataba kati ya TANESCO na IPTL....

Serikali ikubali tu Kenya imecheza rafu kumpoteza waziri wa Fedha...

Nunua Gazeti la Raia Mwema leo...uone jinsi Waziri Wa fedha alivyoshauriana na Waziri Wa Kenya...

Sisi tumeshinda Bomba la mafuta, kenya wanatuchezea rafu kwenye utalii....

Watanzania msiwe wavivu wa kusoma na kujifunza.....kama jambo hulijui....pita hivi

Foreign body wades into tourism tax row

Someni hapo chini News International

Tanzania VAT hike sends safari industry into pandamoneum

New tourism tax roils Tanzania safari industry: Travel Weekly

{{metaTags.other['og:title']}}
 
Maggid nakupongeza kwa kusema ukweli dhahir na serikali naomba iwe na msimamo kwenye jambo hili, vinginevyo tukilegeza hawa makabaila watakua wanatugeuza watakavyo.
Ni kweli Amani ipo, vivutio vipo. Ni suala la kujisimamia kama Taifa naamini tutavuka.
 
Tato wenyewe wamekaa kimaslahi na data za kupika
 

Hapa nadhani mnacholinda ni huo msimamo, lakini sisi tulioko kwenye utalii na tunaojua utalii tumeshaanza kuona kibano chake. Sisi ndio tunakabiliana na watalii na kuwapa ufafanuzi ndio tunajua hii ngoma ya VAT ina makali gani kwa wateja. Wewe na Maggid mnaleta siasa kwenye jambo la msingi kama hili. Kama mmeamua kusimamia kwenye msimamo hapo nitawaelewa, lakini kwenye uhalisia kwenye hilo tumechemsha.
 

Huelewi chochote...unaongea ongea tu

Kenya wana misuko suko...mbona wanatuzidi idadi ya watalii na pesa?
Someni international news

Foreign body wades into tourism tax row

Someni hapo chini News International

Tanzania VAT hike sends safari industry into pandamoneum

New tourism tax roils Tanzania safari industry: Travel Weekly

{{metaTags.other['og:title']}}
 
Kwahiyo VAT ndo tatizo lililoko kwenye tourism?
 
VAT katika Utalii ni jambo la Muhimu sana, Na ninaiunga mkono serikali kwa hatua hii. Kinachotakiwa ni kwa serikali kutoa muda ili wale watalii waliokwisha anza mchakato wa kuja kutalii kabla ya Tarehe 1 July basi waje kwa bei za zamani lakini baada ya hapo Makato ya VAT yaanze.
Ni lazima tupate kipato kwenye utalii. Kama mtu alitaka kuja serengeti atakuja tu asilimia 18 kwa aliyedhamiria siyo kitu
 
Kwahiyo VAT ndo tatizo lililoko kwenye tourism?

Mada ni VAT kwenye utalii, kama ni matatizo yanaweza kuwa mengi, ila kama unataka tukuambie matatizo yaliyoko kwenye utalii fungua uzi huo tutakuja maana hii ndio sekta tunayofanyia kazi.
 
Mada ni VAT kwenye utalii, kama ni matatizo yanaweza kuwa mengi, ila kama unataka tukuambie matatizo yaliyoko kwenye utalii fungua uzi huo tutakuja maana hii ndio sekta tunayofanyia kazi.
Wewe binafsi umekwisha andika makala ngapi kuhusu namna ya kuboresha ongezeko la watalii nchini na mapato kwa ujumla ya taifa.
Nasema hili kwa sababu VAT imewatoa usingizini kwa nguvu zote.
 
Mbona na ww unarukaruka kama mdudu ?

Emu elezea vzur inakuwaje huo mkataba uvunjwe ambao umeufananisha na ule wa dowans na tanesco?

Na tatzo hapa c kodi maana hata kipindi hyo kodi ipo kenya still kenya walifanya vzur zaid ya nyie msio na kodi sasa semen marketing strategies zenu au gvt mziimprovu
 
Mimi nimefanya kazi sector ya utalii ....issue ya VAT imegeuzwa siasa tu ...hii ni moja ya njia ya kubana madalali kulipa kodi. Biashara ya utalii ina mambo mengi na tumepoteza sana mapato sababu ya weakness ya TRA na wizara ya utalii. Mimi naunga mkono VAT kwenye utalii na naamini kama ni kupungua watalii ni kwa kipindi kifupi sababu ya hujuma za madalali lakini baadae tutazoa kodi zetu na utalii kuchangia vyema pato la taifa. Tupunguze sana siasa ...hii ni hatua nzuri sana in long run ...
 
umeandika siasa kwenye mambo yasiyohitaji siasa, siku hizi kila mtanzania ni mwanasiasa, anajihisi anaonewa kwenye kila kitu.. kitu kama hukijui vizuri ni heri kukaa kimya.. hujui wafanyakazi wangapi watapoteza ajira kwenye makampuni ya utalii hivyo kukosa kipato,kisa siasa na ushabiki, wataishije? kuweka VAT kwenye utalii ni kukurupa
 
Hizo ni porojo bana MPadmire

Swali jepesi.

Mwaka jana hii kodi ilikua kenya na tanzania haikuwepo ila kenya bado ilikuwa na watalii wengi zaid ya tanzania
.

Kuna tatizo lipo ila hamlisemi isse c vat hata kdogo kuna zaid ya hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…